Panzermeyer
JF-Expert Member
- Jan 21, 2016
- 471
- 325
Habari wakuu, natumai wote ni wazima. Napenda kuwaletea thread kuhusu Espionage au Intelligence. Espionage ni nini? Espionage ni kitendo cha kukusanya taarifa au nyaraka muhimu za nchi/taifa au taasisi kubwa. Taarifa hizo zaweza kua za biashara, siasa au nguvu ya jeshi la taifa jingine nk na kuzihamisha au peleka sehemu zinapotakiwa kwenda.
Kumbuka kuwa, taarifa hizi hupatikana kupitia njia za kwa siri kwahiyo lazima zifichwe ili yule anayechunguzwa asiweze gundua kile kinachoendelea, na vile vile ni kwa ajili ya kulinda usalama wa taarifa zenyewe, yaani taarifa zifike zikiwa katika ubora unaohitajika.
Thread hii inalenga kuzitaja njia zitumikazo kuhamisha {transmit or communicate} taarifa za kijasusi. Taarifa zikishapatikana zinahitaji kufanyiwa kazi au kuchunguzwa, sasa taarifa haiwezi chunguzwa kama haijafika pale panapostahili.
· Kwa kutumia geresha ya sigara au kiko
Hii njia hupendwa kwasababu si rahisi, katika hali ya kawaida mtu kufikiri kuwa, ndani ya sigara anayovuta spy kunaweza kuwa na ujumbe wa kiintelejinsia. Pia ni njia rahisi kwa usalama wa spy huyo maana kama akigundulika au akishukiwa, basi huweza poteza ushahidi kwa kuuchoma kama vile anavuta sigara.
· Kwa kutumia soli za viatu
Kwenye soli ya kiatu kunakuwa na nafasi ndogo ambayo imetengenezwa (chamber) ili kuweza kuhifadhi taarifa ndogo ndogo. Mfano memory cards zinaweza fichwa hapo. Njia hii ilipendwa sana na warusi maana ilikuwa, japokuwa inaonekana ndogo lakini ina uwezo mkubwa. Memory card iliyofichwa kwenye soli inaweza kuwa na mafile ya picha hadi 500–10000. Au mafaili ya audio records 1000 kutegemea na ukubwa wa device.
· Kwa kutumia michoro (tattoo) kwenye visogo, kisha kuotesha nywele kwenye maeneo hayo ya kisogo upya
Njia hii inatumika kwasababu ya usiri wake. Si rahisi mtu kumshuku spy kama anaweza kua ameficha taarifa kwenye kisogo chake kwa kutumia michoro. Kwaiyo ujumbe au taarifa zinaweza kuonekana pale tu baada ya Spy huyo kunyolewa nywele na kupaka kimiminika ( chemical ) sahihi kisogoni kwake.
· Kwa kutumia macho feki
Hii njia inatumika kwa kuchukua kipande cha kioo ( lenzi ) na kuweka kwenye macho, ila nyuma ya lenzi iyo kuna kua na nafasi ndogo ya kuweza kuhifadhi devices ndogo kama micro chips ambazo zinakua zimehifadhi taarifa muhimu.
· Kwa kutumia sarafu au shillingi
Hii shillingi huonekana kuwa ni ndogo kwa mtazamo, ila zinakuwa na katundu kadogo kadogo ambacho hakaonekani kirahisi, ambacho ukichukua pini na kuipenyeza kwenye ako katundu basi shillingi hiyoinajifungua kati kati au nusu kwa nusu. Katikati unaweza tunza micro chips au memory cards ambayo inaweza kua na taarifa yenye hata kurasa 50 au zaidi.
· Kwa kutumia karatasi maalumu
Hii ni karatasi ambayo, kwa mtazamo inakua tupu yaani haina maandishi kwaiyo sio rahisi kwa mtu kuishuku. Ila ukweli ni kuwa, karatasi hii inakuwa imebeba ujumbe ndani yake. Ujumbe huu huweza kuonekana kwa kuchemsha iyo karatasi kwenye vimiminika vya kemikali sahihi, au maji nk
· Kwa kutumia dead drop
Hapa taarifa hufichwa kwenye eneo ambalo linajulikana kabla au mapema, na baada ya muda mfupi, mtu mwingine anaenda kuzichukua. Njia hii ni maarafu sana na inatumika sana, ni kama zile the most celebrated kamasutra positions hahaha. Faida yake ni kuwa, inazuia nafasi za yule anayeficha taarifa na mpokeaji kukutana uso kwa uso au kuwa wote pamoja kwa wakati mmoja katika eneo husika. Hivyo basi, hata ikitokea muhusika anafuatilia (kama ni double agent ) anaweza akajitetea, na hasa kama eneo lenyewe ni kama kwenye garden, anaweza sema kuwa ameenda kupunga upepo nk.
Taarifa inaweza wekwa kwenye mfuko wa takataka, kinyesi cha ng’ombe au sehemu yeyote ile ambayo itamfanya mpita njia akiona asiweze kupata kishawishi cha kutaka kuchukua au kudadisi hizo taarifa.
· Kwa kutumia mizoga ya wanyama
Mnyama ( panya, paka, sungura nk ) mwenye umbo dogo, ambae yupo hai, anauawa, kisha taarifa za siri zinawekwa ndani yake, anashonwa kwa operation. Baada ya hapo hatua inayofutia ndo muhimu zaidi na ndiyo inayoleta tofauti ( usiri ).
Mnyama huyo hunyunyuziwa vimiminika vya kemikali ambavyo hufanya aoze na kutoa harufu mbaya ambayo ni kero kwa watu na hata wanyama ambao katika hali ya kawaida huwa wanakula jamii iyo ya wanyama (mzoga) kuchukizwa na hyo harufu na kupuuzia huo mzoga, kisha hutupwa kwenye eneo husika au lililokusudiwa ili muhuika wa upande mwingine aweze kuona na kuchukua taarifa hizo.
Kama unafahamu njia zingine, pls share..
Link iyo hapo chini, BBC waki-report maisha ya double agent wao toka anajua recruited mpaka ana deflect. Ni Tanzania tu ambapo inaonekana sio sahihi ila sio uko walipoendelea
Kim Philby, British double agent, reveals all in secret video - BBC News