ESCROW sio siri tena, mambo yote hadharani

Hivi bado CCM wanayo moral authority ya kuongoza nchi hii kweli? Na sijui JPM anajisikiaje kuwa mwenyekiti wa chama kama hiki huku yeye mwenyewe akijivisha joho la mtetezi wa wanyonge. I don't understand.Kwa bahati mbaya sana katika serikali hii bado tunaona dalili za wazi za kuwalinda mafisadi badala ya kuwashuhulikia kwa nguvu zote. Mahakama zipo, mahakimu wapo, mafisadi wapo, nini tatizo? Inakera kwa kweli.
 
Ungetuwekea na kibao cha "Mwanameka" au cisily ya jimmy monimambo.

Chorus imefika na Dj Magu anavyojua ku scratch tuwaangalie kina shabadoo wanavyo breakdance.
 
Duh, yamekushinda leo umeamua uyatapike? Ahsante ila siku zote hukujua au walikunyima ktk mgao? Magufuli fumba macho na masikio uonyeshe kuwa wewe ni "HAPA KAZI TU! " bila kujali yupo nani mbele yako uturudishie heshima ya nchi yetu! Mimi nitaingia 2045 kumalizia yatakayokuwa yamesalia! Tuifanye Tanzania kuwa mahali pazuri kwa kuishi!
 
Kichwa changu hapa nitakionea tu, ngoja nipite na 50 zangu!
 
JK anajua
Ni hivi:- Kaa kimya on escrow tukae kimya kwenye Meli Chakavu ya 1970s inayoozea kwenye Bahari ya Hindi.

"Nitawalinda Wastaafu wote waishi kwa Amani"

Ukitaka kuwa muongo hakikisha unatengeneza cycle kamili ya uongo, lakini ukisema uongo kidogo ukashtuka ukasema ukweli kidgo kisha ukarudia uongo , man sooner rather than later watu wataunganisha dots na kugundua kwamba zinapishana.
Tunakaribia siku ya ukweli kubainika na wote MLINZI na MLINDWA wataadhirika mchana kweupe, it is only a matter of time, and time is ticking quite rapidly!
 
Mmmmmmh, tutatoboa kweli? Mbona kama sioni mwanga mbele? Au macho yangu?
 
Hakika. Kwenye Biblia wanasema kuwa 'msipoongea nitayaamsha mawe kuongea' (unofficial quote).

Mobutu answered (1990s) about corruption in Congo: If you want to steal, steal a little in a nice way. But if you steal too much to become rich overnight, you'll be caught. (my signature)
 
1) Anatafutwa Gavana Prof. Ndulu, 2) kodi kutoka kwa Singa Singa 3) Pesa itakayopatikana ni ya Bombardier nyingine..!! Its a smart movements ila hawa jamaa wanajua kucheza siajabu tukaambulia manyoya!!
Sioni Ndulu akiendelea kuwa hapo BOT jumba la pili expensive hapa Tz
 
Mh Magufuli atawatumbua Sana watumishi wazembe kwa unyonge wao,atawafukuza na kuwa funga Sana watumishi hewa kwa unyonge wao na atawasurubisha Sana wanasiasa wa upinzani kwa Sababu ya unyonge wao lakini hapa kwenye ESCROW ndiyo break yake.

Hata uwe mtakatifu vipi bila kuikataa CCM na kazi zake zote ni lazima ugeuke kuwa mjusi,hata uwe mchapa kazi vipi bila kuikata CCM na kazi zake zote lazima uwe legelege,hata Kama uwe mbishi na mjuaji Sana bila kuikata CCM na kazi zake zote lazima ubadilike na kuwa mtu wa ndiyo mzee na hata kama uwe Moto Sana kiutendaji bila kuikataa CCM na kazi zake zote lazima urudi ukiwa baridi Kama kifaranga cha kuku kilichokosa Joto la mama yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…