- Thread starter
- #21
Hili suala la Escrow lililetwa bungeni hasa na Zitto Kabwe kupitia mgongo wa David Kafulilla ambaye hapo zamani walikuwa maswahiba wa karibu kabla hawajageuziana vibao. Zitto Kabwe alikiri Bungeni kuwa aliwahi kufuatwa na balozi wa Uingereza akiwa na ujumbe wa Standard Chartered Bank (SCB). Japo Bungeni alidai kuwa alitoka nje ya kikao hicho na balozi wa Uingereza pamoja na ujumbe wa SCB, maelezo yake yanatia mashaka makubwa sana. Unaweza kusoma huu uzi "Je, Zitto Kabwe anatumiwa na Standard Chartered Bank?" kwa maelezo zaidi ya hayo madai ya Zitto.
Hili suala lililopeletwa Bungeni, waakina Kafulilla et al wanaojulikana kama "vinara wa Escrow" walikuwa wanataka iundwe "kamati teule" ya Bunge kuchunguza hili jambo na kuja na ripoti yake kama ilivyofanyika kwenye suala la Richmond lakini serikali na wabunge wa CCM wakasisitiza uchunguzi wa hili suala lifanywa na PCCB pamoja na CAG. Baada ya mjadala mkubwa Bungeni hatimaye hili suala likakabidhiwa PCCB na CAG kulifanyia uchunguzi na kuja na ripoti ya uchunguzi huo.
Kwa ufupi hizi "kamati teule" si lolote si chochote zaidi ya kuwageuza Wabunge kuwa ndiyo wachunguzi na matokeo yake inakuwa mwanzo wa biashara ya "blackmailing" kwa wahusika na wajumbe wa hizo kamati wanakuwa wanapiga pesa za nguvu. Ndiyo maana hata baada ya hili jaribio la kutaka kuundwa kwa kamati teule kushindwa, Vinara wa Escrow walikuwa wanahaha kujaribu kushawishi kwanini PCCB na CAG washifanye huo ukaguzi maalum. Unaweza kusoma barua ya Kafulilla kwa Mkurugenzi Mkuu wa PCCB, Dr. Hosea hapa http://www.orcis.com/escrow/Letter_From_Kafulila_To_Hosea.pdf
CAG alipewa "hadidu rejea" (terms of references) kufanya huo ukaguzi na ukaguzi ulifanyika kwa mujibu wa hizo hadidu rejea zilizokubalika pande zote mbili, aliyeomba kutaka huo ukaguzi ufanyike (Serikali/Bunge) na aliyeombwa afanye huo ukaguzi (CAG). Baada ya ukaguzi kukamilika ripoti ya huo ukaguzi uliwasilishwa ofisi ya Bunge na Bunge liliikabidhi hiyo Ripoti kwa Kamati ya PAC. Unaweza kuisoma hiyo Ripoti ya CAG hapa http://www.orcis.com/escrow/Ripoti_ya_CAG_NakalaYaSerikali.pdf
Kamati ya PAC walitakiwa kuiwasilisha Bungeni hiyo Ripoti ya CAG wakiwa na maoni yao. Badala ya kuwasilisha Ripoti ya CAG, walichofanya PAC ni kwenda kuandika Ripoti nyingine kabisa ambayo ni tofauti kabisa na ripoti ya CAG. Ripoti ya PAC unaweza kuisoma hapa http://www.orcis.com/escrow/Ripoti_Ya_PAC_(NakalaYaBunge).pdf
Walichofanya Kamati ya PAC chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe ni kuwaaminisha Watanzania na Wabunge kuwa walikuwa wanawasilisha Bungeni Ripoti ya CAG wakati ukweli ni kuwa walikuwa wanawasilisha ripoti yao mpya kabisa kwa kujificha nyuma ya pazia la Ripoti ya CAG. Ripoti ya CAG ni ripoti ya kitaalamu iliyofanyiwa kazi na kuandikwa na wataalamu, wakati ripoti ya PAC ni ripoti ya kisiasa iliyoandikwa na wanasiasa na ambayo imejaa uongo, udanganyifu, ulaghai na si lolote si chochote isipokuwa ni utapeli wa kisiasa wa kiwango cha juu kabisa.
Unaweza ukasoma UONGO uliokuwepo kwenye Ripoti ya PAC hapa Index of /escrow/viambatanisho Ili kuweza kutambua uongo na utapeli wa kisiasa uliokuwemo kwenye Ripoti ya PAC ni vizuri mtu asome Ripoti nzima ya CAG halafu asome Ripoti nzima ya PAC halafu usome hiyo makala yangu hapo juu. Kushindwa kusoma Ripoti ya CAG na Ripoti ya PAC utakuwa hauelewi uongo na udanganyifu ulikuwepo kwenye Ripoti ya PAC.
Hata baada ya kuwasilisha Ripoti ya PAC hukuwa wakiwaaminisha Watanzania na wabunge kuwa walikuwa wanawasilisha Ripoti ya CAG, PAC ilikuwa imezuia Ripoti ya CAG wasipewe wabunge. Mpaka siku ya pili Bungeni wakati Prof. Muhongo anajibu Ripoti ya PAC, wabunge walikuwa hawajapewa Ripoti ya CAG. Angalia YouTube video hii ambapo Prof. Muhongo anawasilisha majibu ya Ripoti ya PAC iliyowasilishwa na Zitto. Mpaka siku hiyo tarehe 27 Novemba 2014, Wabunge walikuwa hawajapewa Ripoti ya CAG. Kamati ya CAG kwa makusudi ilikuwa inahodhi na kuzuia Ripoti ya CAG isiwafikie wabunge. Sikiliza kuanzia dakika ya 7 ambapo Wabunge wanapiga kelele kwanini hawajapatiwa Ripoti ya CAG.
Ndiyo maana hata JK aliporudi kutoka Marekani alitoa agizo kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani watu wote waisome. Kitendo hichi cha JK kilimkera sana Zitto Kabwe na genge lake la "Vinara wa Escrow". Waulizwe kwanini walikuwa wanaificha Ripoti ya CAG?
Shukrani mkuu kwa uchambuzi wako. Huu ndo uzuri wa ukweli hupenya vikwazo vyote na kubaki wazi tofauti na uongo ambao hauna uwezo huo.