ESCROW na Makandokando yake

ESCROW na Makandokando yake

kalikenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Posts
1,649
Reaction score
373
Ni takribani zimepita siku tatu tangu kumalizika kwa kikao cha bunge la JMT kule Dodoma huku Taifa likiwa limeachwa kwenye sintofahamu ya.kushindwa kuujua ukweli wa nini hasa kilichojiri kwenye akaunti ya Escrow. Ili kuielewa sintofahamu hii nitatumia mfano wa tukio la kweli lililotolea mtaani kwetu jana.

Majira ya saa tatu za isiku tulisikia kelele za mwizi ambapo wengi wetu tuliokuwa majumbani tulitoka na kila aina ya silaha kwa lengo la kumtia adabu.huyo mwizi. Kulikuwa na vijana watatu wanakimbia. Nasi bila ya kuhoji tukaanza kuwapiga wale vijana japokuwa walikuwa wakijitetea kuwa hawakuiba. Tuliendelea kuwasulubu hadi walipoonekana kuwa wameiva kwa kichapo, kuna mzee wa makamu akatuasa kuacha kuwapiga na kuuliza ni nani aliyeibiwa na wameiba nini. Swali lile lilionekana kutushtua kwani ghafla kila mtu alijihisi kuwa na hatia na hivyo kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria, tulianza kupotea eneo la tukio kabla mambo hayajaharibika.

Ni tukio hili ndo limenisukuma kukumbuka makandokando yaliyolizunguka sakata la Escrow.

Kama tukumbakavyo sakata hili liliibuliwa na David Kafulila ambapo alikwenda mbali.zaidi kwa kumuita AG Werema kuwa ni mwizi ambapo reaction ya werema ilikuwa ni kuibuka kwa matumizi mapya ya msamiati wa Tumbili.

Pia kutokana na kuibuka kwa sakata hilo, Bunge lilimuagiza CAG kufanya ukaguzi wa dharura kwenye akaunti ya Escrow na kiwasilisha taarifa hiyo. Sio jukumu langu kurudia tulioyasikia na kuyaona.

Lengo langu ni kuwashirikisha wanajf juu ya kile ninachohisi kuwa ni makandokando yaliyopo nyuma ya sakata hili kwa nia njema ya kutumia jicho la tatu.

Na haya ndio makandokando ya Sakata zima la ESCROW.

Kwa muda wote wa sakata hili, tuliaminishwa kuwa Werema, Muhongo, Maswi na Pinda ni miongoni mwa walionufaika na fedha za Escrow. Lakini kwa mujibu wa taatifa ya CAG hawajaoneshwa kuwa kuna miamala inayowahusu.
Upi ukweli kuwa waliiba au hawakuiba? Lakini jambo la kushangaza ni kuwa kwa mujibu wa Mwigulu Nchemba, suala zima la Escrow ni purely legal and technical issue na sio political.

Kwa mujibu ws maelezo ya wabunge na media, kuna mkanganyiko kuhusu fedha zilizodaiwa kuibwa ni takribani Bil 306, 321 na Bil 183. Lakini hadi Bunge limaweka maazimio kiasi halisi kilchokuwemo kwenye akaunti hiyo hakijulikani.

Ripoti ya CAG ilikuwa haijitoshelezi na badala ya kuagiza ukaguzi wa kina, PAC ilikurupuka kuwa DPCCB na mkurugenzi mkuu wa TRA watoe maelezo mbele ya Kamati ambao pia hawakuwa na majibu yanayojitosheleza kuwa fedha za Escrow ni umma au ni za IPTL Hapa inatoa mashaka kuwa taarifa ya CAG haikuwa conclusive ma hivyo kuhitaji corroborative evidence. Mtu kama DPCCB hakustahili kuitwa kwa kuwa hakuwa sehemu ya uchungiuzi.

Mjadala kugubikwa na jazba na kelele na vitisho. Kwa kawaida jambazi akitaka kuchukuwa kitu hutumia vitisho na nguvu. Na mwanasiasa yeyote akitaka jambo lake lipite hutumia pia vitisho na uibuaji wa kashfa na wakati wa kujadili hujitahidi kuonesha jinsi alivyoguswa na uovu anaoulalamikia. Hili lilijitokeza kwa kiwango cha juu kiasi cha kuanza kutuaminisha kuwa nyuma uzalendo kuna jambo lililojificha. Hili linathibitishwa na aina ya maazimio yaliyopendekezwa na PAC. Kama sio hivyo ni kwa nini mjadala haukuwa ma busara?

Kutokana na makandokando haya, itakuwa ni jambo la busara iwapo raisi haitaingia kwenye mkenge na badala yake awarudishie bumge suala hilo ili waagize ukaguzi wa kina kufanyika

Karibuni kwa mjadala.
 
Hapa najua wanywa viroba hawatii mguu labda matusi.
 
Ni wazi kuwa Thread hii imewachoma waliotumia ufisadi kupambana na ufisadi.
 
Kalikenye, naunga mkono hoja yako na nadhani kuna ya kupiga kelele ili ufanyike uchunguzi wa kina ili tuhuma za kishabiki zilizotolewa zifanyiwe uchunguzi ili kubaini kilichopo nyuma yake.
 
Haamna kujdiliana hapa, inalekea na wee ulimegwa.
 
Inaonekana thread za kupinga uhuni wa PAC leo ni nyingi.
 
Kuna kazi ambazo kamati husika ingezisimamia tungeweza kuona tuna kamati inayotaka kuona Bunge linaheshimiwa lakini si haya mengine.

Wakati mwingine huwa nasikitika kuzaliwa mtanzania!
 
Nimejifunza kuwa mada serious huwa hazina wachangiaji wengi.
 
Hili suala la Escrow lililetwa bungeni hasa na Zitto Kabwe kupitia mgongo wa David Kafulilla ambaye hapo zamani walikuwa maswahiba wa karibu kabla hawajageuziana vibao. Zitto Kabwe alikiri Bungeni kuwa aliwahi kufuatwa na balozi wa Uingereza akiwa na ujumbe wa Standard Chartered Bank (SCB). Japo Bungeni alidai kuwa alitoka nje ya kikao hicho na balozi wa Uingereza pamoja na ujumbe wa SCB, maelezo yake yanatia mashaka makubwa sana. Unaweza kusoma huu uzi "Je, Zitto Kabwe anatumiwa na Standard Chartered Bank?" kwa maelezo zaidi ya hayo madai ya Zitto.

Hili suala lililopeletwa Bungeni, waakina Kafulilla et al wanaojulikana kama "vinara wa Escrow" walikuwa wanataka iundwe "kamati teule" ya Bunge kuchunguza hili jambo na kuja na ripoti yake kama ilivyofanyika kwenye suala la Richmond lakini serikali na wabunge wa CCM wakasisitiza uchunguzi wa hili suala lifanywa na PCCB pamoja na CAG. Baada ya mjadala mkubwa Bungeni hatimaye hili suala likakabidhiwa PCCB na CAG kulifanyia uchunguzi na kuja na ripoti ya uchunguzi huo.

Kwa ufupi hizi "kamati teule" si lolote si chochote zaidi ya kuwageuza Wabunge kuwa ndiyo wachunguzi na matokeo yake inakuwa mwanzo wa biashara ya "blackmailing" kwa wahusika na wajumbe wa hizo kamati wanakuwa wanapiga pesa za nguvu. Ndiyo maana hata baada ya hili jaribio la kutaka kuundwa kwa kamati teule kushindwa, Vinara wa Escrow walikuwa wanahaha kujaribu kushawishi kwanini PCCB na CAG washifanye huo ukaguzi maalum. Unaweza kusoma barua ya Kafulilla kwa Mkurugenzi Mkuu wa PCCB, Dr. Hosea hapa http://www.orcis.com/escrow/Letter_From_Kafulila_To_Hosea.pdf

CAG alipewa "hadidu rejea" (terms of references) kufanya huo ukaguzi na ukaguzi ulifanyika kwa mujibu wa hizo hadidu rejea zilizokubalika pande zote mbili, aliyeomba kutaka huo ukaguzi ufanyike (Serikali/Bunge) na aliyeombwa afanye huo ukaguzi (CAG). Baada ya ukaguzi kukamilika ripoti ya huo ukaguzi uliwasilishwa ofisi ya Bunge na Bunge liliikabidhi hiyo Ripoti kwa Kamati ya PAC. Unaweza kuisoma hiyo Ripoti ya CAG hapa http://www.orcis.com/escrow/Ripoti_ya_CAG_NakalaYaSerikali.pdf

Kamati ya PAC walitakiwa kuiwasilisha Bungeni hiyo Ripoti ya CAG wakiwa na maoni yao. Badala ya kuwasilisha Ripoti ya CAG, walichofanya PAC ni kwenda kuandika Ripoti nyingine kabisa ambayo ni tofauti kabisa na ripoti ya CAG. Ripoti ya PAC unaweza kuisoma hapa http://www.orcis.com/escrow/Ripoti_Ya_PAC_(NakalaYaBunge).pdf

Walichofanya Kamati ya PAC chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe ni kuwaaminisha Watanzania na Wabunge kuwa walikuwa wanawasilisha Bungeni Ripoti ya CAG wakati ukweli ni kuwa walikuwa wanawasilisha ripoti yao mpya kabisa kwa kujificha nyuma ya pazia la Ripoti ya CAG. Ripoti ya CAG ni ripoti ya kitaalamu iliyofanyiwa kazi na kuandikwa na wataalamu, wakati ripoti ya PAC ni ripoti ya kisiasa iliyoandikwa na wanasiasa na ambayo imejaa uongo, udanganyifu, ulaghai na si lolote si chochote isipokuwa ni utapeli wa kisiasa wa kiwango cha juu kabisa.

Unaweza ukasoma UONGO uliokuwepo kwenye Ripoti ya PAC hapa Index of /escrow/viambatanisho Ili kuweza kutambua uongo na utapeli wa kisiasa uliokuwemo kwenye Ripoti ya PAC ni vizuri mtu asome Ripoti nzima ya CAG halafu asome Ripoti nzima ya PAC halafu usome hiyo makala yangu hapo juu. Kushindwa kusoma Ripoti ya CAG na Ripoti ya PAC utakuwa hauelewi uongo na udanganyifu ulikuwepo kwenye Ripoti ya PAC.

Hata baada ya kuwasilisha Ripoti ya PAC hukuwa wakiwaaminisha Watanzania na wabunge kuwa walikuwa wanawasilisha Ripoti ya CAG, PAC ilikuwa imezuia Ripoti ya CAG wasipewe wabunge. Mpaka siku ya pili Bungeni wakati Prof. Muhongo anajibu Ripoti ya PAC, wabunge walikuwa hawajapewa Ripoti ya CAG. Angalia YouTube video hii ambapo Prof. Muhongo anawasilisha majibu ya Ripoti ya PAC iliyowasilishwa na Zitto. Mpaka siku hiyo tarehe 27 Novemba 2014, Wabunge walikuwa hawajapewa Ripoti ya CAG. Kamati ya CAG kwa makusudi ilikuwa inahodhi na kuzuia Ripoti ya CAG isiwafikie wabunge. Sikiliza kuanzia dakika ya 7 ambapo Wabunge wanapiga kelele kwanini hawajapatiwa Ripoti ya CAG.

Ndiyo maana hata JK aliporudi kutoka Marekani alitoa agizo kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani watu wote waisome. Kitendo hichi cha JK kilimkera sana Zitto Kabwe na genge lake la "Vinara wa Escrow". Waulizwe kwanini walikuwa wanaificha Ripoti ya CAG?
 
Back
Top Bottom