ERROR 77

Hackerz

JF-Expert Member
Apr 25, 2016
352
235
JINSI YA KUONDOA ERROR 77 KWENYE MITA ZINAZOANZA NA NAMBA 2421...*

*ERROR 77*

Hii ni error ambayo inapatikana kwenye mita tengano maarufu kama mita za rimoti au CIU ambazo zinafungwa juu ya nguzo na zinaanza na namba ya mita 2421.....

*NINI KINASABABISHA ERROR 77*

*Error 77* inamaanisha kuwa mita yako ya kwenye nguzo na rimoti yako hazina mawasiliano hivyo umeme hauwezi kuingia. Mara nyingi inatokea unapotaka kuweka umeme baada ya kuisha unit.

*JINSI YA KUTATUA ENDAPO ITATOKEA*

Unatakiwa kuhakikisha kuwa umeme kwenye mtaa wako upo na kama nyumba yako haina umeme yaani unit zimeisha weka betri zenye nguvu kwenye rimoti yako na kisha fata taratibu zifuatazo

1. Zima switch zote za nyumba yako, *hakikisha zote zimezimwa*

2. Washa switch moja tu ya ukutani na chomeka hiyo rimoti kisha bonyeza zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako alafu tena zero(0) ikifuatiwa na mita namba yako kisha bonyeza ok au enter..

*Mfano mita namba yako ni 241234567 Utafanya ifuatavyo *024212345670241234567ENTER*

3. Baada ya kubonyeza ok itaakuandikia *GOOD* apo sasa weka umeme wako kama kawaida na utapata umeme.

*ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA ZA TANESCO*
 
Back
Top Bottom