PreGE2025 Eric Shigongo: Rais Samia kutoa Billioni 8 kujenga kivuko kipya na kuongezeka kwa vivuko vinne Buchosa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameishukuru Serikali kwa kutoa vivuko vinne vitakavyotoa huduma za usafiri kwa wananchi wa Buchosa

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata nne zinazounda Kisiwa cha Kome, kilichopo katika Jimbo la Buchosa

Shigongo ametaja vivuko hivyo kuwa ni MV Sengerema, ambacho kitatoa huduma za usafiri kwenye visiwa vya Kasalazi, Gembale hadi Kisiwa cha Soswa

Vingine ni MV Mwanza, MV Kome II, na MV Kome III, ambavyo vyote vitatoa huduma za usafiri kati ya Nyakaliro na Kisiwa cha Kome, Jimbo la Buchosa

Mbunge Shigongo amesema wananchi wa Buchosa wanapaswa kutembea kifua mbele kwa kupata vivuko na miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika jimbo hilo


Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…