Epuka majuto utu uzima ukifika

Epuka kuwa masikini uzeeni, mke na watoto wataungana kukupa simanzi
Kwa sisi wanaume ukishafika ule umri basi jua upo mwenyewe maana hawa wenzetu huwa wanakuwa hawaoni umuhimu wetu tena umri wa kustaafu ukifika ukawa tu upo idle wanakuona ni takataka.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hii ya kutembelea makaburi hapana ndugu. Mambo ya kuishi huku unawaza kufa mimi huwa siyapendi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hata kama ni wewe ungechagua kukijiajiri wakati kuna mshahara wa 30,000 bank wakati serikalini wanalipana sh. 3000?
Kujiajiri imekaa kimkakati zaidi. Yaani unaweza jiajiri kwa malengo ya muda mrefu so unaanza kujifunza mambo mbali mbali mdogo mdogo huku ukichukua experience.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sisi wanaume ukishafika ule umri basi jua upo mwenyewe maana hawa wenzetu huwa wanakuwa hawaoni umuhimu wetu tena umri wa kustaafu ukifika ukawa tu upo idle wanakuona ni takataka.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Thus ukifika miaka 50 andaa maisha YAKO Shamba kaishi na wafanyakazi waache wao waishi mjini mwenye hamu aje mwenyewe akusalimie
 
Thus ukifika miaka 50 andaa maisha YAKO Shamba kaishi na wafanyakazi waache wao waishi mjini mwenye hamu aje mwenyewe akusalimie
Yeah unatakiwa kuwa na miji miwili m'moja ambao utaishi na mkeo halafu huo mwingine utaishi wewe pekee yako na mkeo asijue maana guaranteed atataka ahodhi uwe mali yake.

So akianza tu kukuletea za kuleta, wewe unasepa bila kelele. Unamuacha aishi anavyotaka. Wanaume uzeeni huwa wana athiriwa na vitu vya kipuuzi sana ndivyo huwapa stress za kuwanyima raha.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Noted Mkuu,
Ongeza pia, suala la kumtumikia Mungu mmoja wa kweli,
Maana bila hivyo ni ngumu Sana kufanikiwa,
Unamaanisha nini kufanikiwa?? kuwa na pesa ama mafanikio mengne, na kama ni mengne yataje tafadhali!
 
Eeh tembelea makaburi tena??!!😲😲😲😲 Mwisho utakuwa mchawi.
Kwani ukisoma quran na bible sii tayari vina kukumbusha kuwa dunia tunapita
 
Umeandika "Ngera" tupu. Elewa tu kwamba maisha ni fumbo. Mambo ya kukariri kwamba miaka hii fanya hiki, mwaka hii fanya kile, tuwaachie wanafunzi wa english medium.
 
Unaweza kuwa umetulia zako, uko bize tu na mambo yako mara ghafla unakumbuka umri wako.... AAARGHHH yaani mood inakata ghafla..
 
Kwa utafiti wangu niliofanya huko Mabibo unaonyesha kwamba mtu anayeandika maandishi mengi sana bila kufupisha anakuwa na stress ya umri. Ndugu yangu usijali tuko wengi kwenye hii boti YA UMRI. Cha muhimu tuzingatie amri za Mungu na malezi ya wazazi/walezi wetu. Ukiwa mcha Mungu hayo mambo mengine yote yanajiseti yenyewe. Hakuna kuwahi wala kuchelewa maishani.
 
Aisee maisha sio mchezo ,vijana wakiwa vyuoni hawawezi kuelewa mpaka waje waicheze Nii ngoma ndio huelewa!!?
Fikiria una maliza chuo unalate 20s Kisha una pambania na ajira ikifika 35 inabidi uoe!! 36 unapata mtoto,38 unapata mtoto .
Unagonga 40 dogo anataka shule ( basi la njano) baada ya miaka minne mdogo wake anataka shule ( wewe una 44)daaah ukifika 47 wanataka sekondari !!! Ukifika 50+ wanaliza sekondari!!Bado miaka kumi kustaafu!! Daaaaah!! Bado untakiwa uwe umejenga na maisha yaendelee!! Hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…