EPL na changamoto za Video Assistant Referee(VAR)

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu Habari zenu?

Kwenye EPL swala la kutumia VAR kumekuwa na malalamiko mengi kuwa VAR inaonekana wengine inawapendelea na wengine inawahumiza, na kuna wengine wanapendelewa zaidi kutoka na maamuzi yanayotolewa kila mechi wao ndio wanapata faida na VAR.

Kwa maoni yangu VAR ya EPL isiwe inafanya maamuzi ya kuamua, wamuachie refa ndio atoe maamuzi kulingana na yeye alivyoona kwenye marudio ya tukio pembeni kwenye video.

kama ilivyokuwa kwenye mechi za UEFA Champions League au club bingwa dunia faulo au offsides zote zenye utata refa anaenda kuangalia marudio kwenye video yeye mwenyewe.

refa ndio atakaye amua Baada ya kuangalia marudio ya Tukio na sio kupewa maamuzi kama kwa sasa wanavyofanya kwenye EPL, ndio maana baadhi ya timu zinaonekana kubebwa na maamuzi ambayo sio Sawa kulingana na maamuzi Yaliotolewa .mpira ni mchezo wa hadharani kila mtu anaona kweupe.

Kwenye EPL sijaona umuhimu wa kuweka watu Wakufanya maamuzi tofauti na refa pale uwanjani.
Kwenye EPL, VAR imekuwa ni kioja unachezewa faulo wewe var inasema eti wewe ndio umefanya faulo.

Huu mpira atuja anza kuangalia leo na sheria tunazijua kama faulo au offside wakifanya replay inaonekana kabisa.

IMG_8396.jpg


Ni hayo tu Wakuu.
 
Back
Top Bottom