Enziiii za Mwalimu

mimi hata sielewi kwanini kikwete anashindwa kuwaunganisha watanzania naona kama tatizo ni dogo sana na ana uwezo kabisa wa kulirekebisha ila tu hataki au amekua mwoga!yaani nguvu ya pesa imemtawala zamani tuliishi maisha ya raha sana tulipendana na kuheshimiana kama ndugu kuliko sasa mwenye pesa ndiye anayeheshimika!
tutamkumbuka sn mwalimu kwani alikuwa na akili nying na ali2uunganisha watz kupitia shule sio huyu kijeba kikwete anayewagawa watz kwa ari zaid nguv zaid na kasi zaid kupitia dini na shule za kata
 

mkuu nilikua songea kuanzia 84 mpaka 86 nikahamia morogoro. nilikwepo SONGEA wakati maji maji ipo juu na kulikuwa na timu ya RTC wakati ule ilikuwa ligi daraja la pili. namkumbuka deadly striker wao akiitwa KIDIMBE goalie akiitwa JORDAN ne beki mbili yao akiitwa NDUMBARO. Wacha ya majimaji hii RTC ILIKUWA saafi saana jamaa walikuwa wanajifua kuanzia saa tisa mchana jua kali ikifika saa kumi na mbili mazoezi yameisha. timu ya wahuni pale mjini ilikuwa inaitwa OLYMPIC wapiga ganja wote wa town walikuwepo hapo so wakati wa bogota sikwepo. nikirudi tena kunyumba 95 nikakuta timu mbili pale town wauza mitumba wakijiita business au biznesi na timu nyingine ikiitwa MCHELE wafanya biashara ya mchele haoo zote zilikuwa ligi daraja la tatu. primary raha nyie acheni tuu pale JANGWANI primary sumbawanga nikiwa kwenye timu ya darasa la pili kila mapumziko tunacheza na std three sasa kuna jamaa alikuwa std three akiitwa evodi jamaa alikuwa anapiga chenga balaa na watu waliamini huwezi kumpiga chenga kuna siku tuliwapiga bao tatu mbili bao la ushindi nililipiga mwenyewe baada ya kumpiga chenga evodi na kumfunga golikipa goli la tobo sitisahau ile siku ilibadilisha kabisa muonekano wangu darasani.
 
kipindi hiko nipo mtwara shule ya ligula dah...mapumziko ya saa 4 mnachangachanga shimkumi'kumi mnaenda kula kashata na mabumunda,dah kuna jamaa mmoja akiitwa abilah,dah jamaa alikuwa m-babe kinoma,ye akibonda shule nzima,yaani ye mademu wote wake,alikuwa yeye haji na fagio,kwa iyo tunamchotea hadi fagio wake unakuwa mkubwa kuliko wote,na kuhusu kuwwahi namba ni lazima mtu achukue namba 2 moja ilikuwa yake...duh...tukishaanza 1 tach ile kengele ya madarasani ilikuwa inaniuzi kinyama...ila kikubwa ni kwamba najiuliza hivi kwanini wale jamaa wakiojifanya wababe,wanabonda shule nzima walikuwa vilaza sana,kwanini??yaai swala la mitihani likija tu,wao macho juujuu tu,majibu yakija ni namba za viatu tukama sio zero kabisa!!!khaa so fun enz zile
 
umenikumbusha timu ya mchele ni kweli ilikua darala la tatu halafu unamkumbuka celestine sikinde mbunga na dadi athman enzi hizo majimaji ilikua juu sana ilitoa vipaji vingi unajua kipindi kile kulikua na umisseta na umitashumta na umisavuta pia yaani michezo ilikua mingi sana sio kama sasa siasa zimetawala!
 
hivi ni mwaka gani ule meimosi kitaifa ilifanyikia mtwara?miaka ile viongozi walikua na nidhamu sana
 
Enzi za Mwl. ilikuwa tambarare sana, tulikuwa tunapelekwa kumpokea Mwl. saa nne barabarani na matawi ya miti, hatutoki mpaka anapopita saa kumi! Sasa hivi Mkwere anapita kama msanii, hakuna kumaind.

Nakumbuka viatu vizuri ukivaa ni raba za Bora Shoe na Chachacha!

Ila nilikuwaga napenda mchezo wa "tali bado" sijitokezi na ... mpaka nimetosha!
 

Hahahaha! Dah mzee umenikumbusha mbali sana, Hizo bora shoes nilizivaa sana mpaka kuna wakati nilichezea mpira kabisaaa kwenye mechi ya darasa na darasa na chachacha nilizivaa sana nikienda kucheza watoto wenzangu, dah yale maisha yalikuwa matamu sana aisee!

Natamani atokee Kiongozi mwenye mawazo kama ya Kinyerere vile atengeneze mfumo wa maisha matamu kama enzi za mwalimu. Kweli UTU una thamani zaidi kuliko PESA.
 
sana nakuunga mkono sana man
 

du!!!umenikumbusha mbaaaali,nakumbuka enzi za kuhesabu vema na vizuri kwenye daftari!!!na walimu hawakuwa wachoyo wa kutoa hizo vizuri na vema!
 
Wakucheza mpira kama una viatu hauruhusiwi. Wote lazima muwe peku
 
hahaaaaaaa unaesabu tiki na vema pia kipindi kile mwalimu alikua anakaririsha table sana akiingia tu na bakola yake utasikia kilimasela tebo ya 7 duh nilikua napenda sana table ya 12 na 10 na ya 11 kwasababu zilikua rahisi sana
du!!!umenikumbusha mbaaaali,nakumbuka enzi za kuhesabu vema na vizuri kwenye daftari!!!na walimu hawakuwa wachoyo wa kutoa hizo vizuri na vema!
 
unakumbuka shule za msingi zilikua na bendi na ngoma na filimbi mpaka matarumbeta basi sikukuu za kuzaliwa chama,mapinduzi ya zanzibar uhuru wa tanganyika nk ilikua raha tupu maandamano wanafunzi na wafanyakazi tulikua kitu kimoja!
 


Mkuu umenikumbusha mbali mno maana tulikuwa tunakwenda na mahindi ya kuchemsha, karanga za kuchemsha na viazi vitamu vya kuchemsha

Zamani raha kweli siku hizi watoto wanakwenda na sausage na juicy enzi hizo vitoke wapi?? Pilau mpaka Christamas na Mwaka mpya au Pasaka
 
hapo sasa kwa mchanganyiko huo wa vyakula tumbo likijaa gesi mabomu utakayoyaachia class kila mtu atakimbia anakuachia dawati peke yako!
 

umesoma kanda ya ziwa?
 

duh nimecheka leo mpaka machozi yananitoka jamani JF burudani kwa kweli sijuti kujiunga nayo dah.asante chimunguru kwa stor tamu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…