Enzi za utawala wa mwalimu J.K na hili la Gwajima kwa Pengo.

Enzi za utawala wa mwalimu J.K na hili la Gwajima kwa Pengo.

chizoza

New Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Habari wakuu nimetafakari nimekosa majibu hivi hili tuko la Gwajima angelifanya enzi za mwalimu Nyerere unahisi ni kitu gani au ni maneno gani ambayo mwalimu angeweza kuyasema juu ya Gwajimaa? mawazo yenu muhimu hapaa.
 
Mwalimu, angemnunulia PEPSI baridi.
 
Habari wakuu nimetafakari nimekosa majibu hivi hili tuko la Gwajima angelifanya enzi za mwalimu Nyerere unahisi ni kitu gani au ni maneno gani ambayo mwalimu angeweza kuyasema juu ya Gwajimaa? mawazo yenu muhimu hapaa.

Duh...!.
Japo siungi mkono kauli hizi za Gwajima kumtukana Pengo, ila
Wanabodi, kwenye siasa, hakuna rafiki wa kudumu, wala adui wa kudumu, kuna just common interest.
Japo katika bandiko hili, nilitofautiana na Gwajima, lakini kufuatia kwa sasa ni mimi ni kada, na mgombea aliyepitishwa na chama chetu kwa jimbo la Kawe ni Gwajima, naomba kudeclare kuwa sasa namuunga mkono Gwajima 100% kwa 100% nikalikomboe jimbo, tulirejeshe CCM!.
Mimi na Gwaji Boy...dam dam!.
P
 
Mkuu Pascal, umeongea kitu ambacho mimi naona ni tatizo kubwa sana Tanzania, kufikia mahali nimsema sana kwamba tatizo tulilo Tanzania na nchi masikini ni kuwa na watu wenye akili ndogo kama viongozi, eidha kwa kuteuliwa au kuchaguliwa kwa kura.

Frankly speaking, msimamo unaouweka wazi hapa mie naona kama ni political illiteracy, kwamba tuko tayari hata kumuunga mkono mwendawazimu ambae hataweza kuisaidia Tanzania katika maendeleo yetu, ili mradi tu ni mwanachama wa chama tunachoshabikia?

Hii ni partisanship of the stupidest order, ambayo mimi naona kama tunakuwa hivyo basi hatuna akili sawasawa na tunapaswa kuhurumiwa sana. Ni lazima watu tuelewe kwamba Tanzania is so much bigger than our Mickey Mouse political parties ili tuweze kuendelea, la sivyo tuondoe mfumo wa vyama vingi maana unakuwa counter productive, hautimizi objectives za kuuanzisha. What Nyerere had in mind aliposema tuanzishe mfumo wa vyama vingi sichi hiki kinachoendelea Tanzania.

Ni lini tutawachagua watu kutokana na sifa zao za kuwa voingozi badala ya kuwachagua kwa kuwa wako kwenye chama tunachoshabikia, no matter kiwe kinafanya upumbavu gani?

Ni lini tutaona maoni mazuri juu ya nchi yetu ni mazuri regardless yanatolewa na mtu wa chama tunachoshabikia au la?

NI lini upumbavu kwetu utakuwa ni upumbavu hata kama unafanywa na chama cha siasa tunachoshabikia?

Ni lini tutaacha kumshabikia na kumtetea Lowasa kwa kuwa yuko chama chetu, kumtukana kwa kuwa kahamia upinzani, na kumshabikia kwa kuwa karudi chama chetu? Huu ni unafiki ambao mtu yeyote mwenye akili ataelewa.

Ideallly, ningependa kuona Magufuli na Lissu wote wakiwa viongozi wa serikali ya Tanzania, kwa kuwa wao kuwa katika vyama tofauti ni missed opportunities kwa maendeleo ya nchi yetu. Ndio maana nakuambia it is better tuondoe mfumo wa vyama vingi. Watanzania we are just too immature, politically illiterate kuwa na siasa za vyama vingi. Hata nikiwa mbele ya Magufuli nitamwambia hata yeyey yuko too immature kuwa raisi katika mfumo wa vyama vingi. Hata Ndugai, Tulia, Kabudi nk. Majaliwa ana nafuu. Sijui Lissu, I may not be able kum-judge kwa sasa.
 
Back
Top Bottom