Jamaa mmoja alimwambia mkewe
"Honey unaonaje tujikumbushe zile
enzi za uchumba wetu?"
Mke akakubali kwa kusema " Sawa si
vibaya" Jamaa akamwambia mkewe
"Basi kesho tukutane saa 4 garden"
Mke akakubali.
Siku ya pili Jamaa akafika garden
akamsubiri sana mkewe kwa masaa
mawili lakini hakutokea.Aliporudi
nyumbani akamuuliza "Mbona
hukutokea? Mke akajibu "Mama
alinikataza nisitoke"