Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Kwanza nachukua fursa hii kuwa pongeza Mh. Mbowe na team yake kwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Ghana, mme fanya vyema sana, maana aliyeshinda ni mpinzani na hivyo atawapeni mbinu zilizomsaidia kushinda.
Tunashinda kutoka kwa waliojifunza na kushinda, yaani tunajifunza kutokana na masahihisho, hivyo msitoke bure huko Ghana bila kupata chochote cha kujifunza ili kupata Experience ya mpinzani ambaye sasa amekuwa mtawala. Wakati mnapata mbinu mpya huko Ghana, nami nitawaleteeni mbinu 30 za kuingia madarakani kiulani na kuiacha CCM ina mbwaya mbwaya.
Msijali mimi niko kwa ajili ya kuwajenga maana ninyi najua mlivurugwa ndio maana mkanichukia lakini ukweli umeshajulikana. NAWAPENDA SANA mimi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.
MBINU 30 ZENYEWE NDIO HIZI HAPA;
kuanzia sasa mpaka kufikia 2020 fanyeni yafuatayo:
1. Someni matamko yote, makala zote, vitabu vyote vya Deogratius Kisandu tokea mwaka 2009 mpaka Leo. Na kisha fanyieni kazi kimoja baada ya kingine.
2. Tafteni clips zote za interview za TV na Radio za Deogratius Kisandu na fatilieni hoja zote na kuzifanyia kazi.
3. Tafteni clips zote za kampeni na mikutano ya hadhara ya Deogratius Kisandu, kuanzia akiwa CDM, NCCR Mageuzi na mkutano mmoja wa kujiunga CCM. Mtapata mahali pa kuanzia kama chanzo.
4. Angalieni mnaoshindana nao wanafanya nini kwasasa, na ninyi fateni mlemleeee. Hii inaitwa ngoma droo.
NJIA YA 5-12 YA UPINZANI KUIONDOA CCM 2020.
Baada ya kuangalia njia ya 1-4, sasa tuangalie njia zingine tena:
5. Tume huru, kama tume haitakuwa huru basi hakikisheni iwe Tume ya Kidemokrasia.
6. Matokeo ya Uchaguzi yasitangaziwe kituo cha Polisi. Pelekeni hoja bungeni ili utaratibu wa uchaguzi uzingatiwe.
7. Jeshi la Polisi ni Mali ya wananchi hivyo fanyeni kazi na jeshi kwa urafiki.
8. Mawakala wawe wale ambao hata asipopewa kitu atajitolea. Anzeni kuwatengeneza bado mapema(wafia chama).
9. Kama tutapiga kura Electronic basi msikubali kuhesabu Hard copy. Itakula kwenu.
10. Wanawake hutumika sana kuangusha Upinzani, hivyo kuweni makini na anzeni kuwa elimisha na kuwakanya.
11. Asasi za kiraia na kidini kuweni ndugu zao bila mamlaka.
12. Kilichomuokoa Quattara ni kuwa na Mwanasheria Mkuu wa Upinzani jasiri aliyemuapisha kuwa Rais, wakati yule wa SERIKALI alimwapisha Rais Bagbo ambaye alinyang'anywa mamlaka baadae. Chukueni hii.
NJIA YA 13-15 UPINZANI KUIANGUSHA CCM 2020.
Tunaendelea na upambanuzi wa namna tunavyoweza kushika dolla 2020:
13. Msikubari watabiri uchwara, wengi hupewa pesa kabla au kushinikizwa kutoa majibu yasiyo sahihi au kwa upambe au kwa propaganda. Kumbuka siku hizi Mungu amegeuzwa biashara. Mnauwezo mkubwa wa kujitabiria wenyewe kama mkiwa vizuri rohoni.
14. Msiongelee mambo makubwa, chukueni Yale ya kipuuzi ambayo ndio tija na myafanyie kazi hasa. Operesheni zinahitaji mambo ya msingi na sio mafisadi na rushwa.
15. Wekeni Viongozi (sio lazima Vijana) wenye ushawishi au umakini au wajuvi wa mambo wawepo kila MTAA, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na taifa ili kukabiliana na hoja za upande wa mshindani.
NJIA 16-20 UPINZANI KUIPOROMOSHA CCM 2020.
Unajua waheshimiwa msiogope vyeo, ogopeni Kiongozi mwenye Hekima. Tunaendelea na njia zingine tena:
16. ielezeni jamii Ukweli wa maovu wanayofanyiwa ili wawe hivyo walivyo. Najinsi ya kujinasua. Unajua unaweza kulipwa mshahara wa milioni 3 kwa mwezi lakini ukaishi katika mateso na mshahara wako. Unaweza kupewa mikopo ya riba nafuu lakini ukarejesha kwa mateso. N.k
17. Katiba Mpya isiwe hoja, Bali hoja iwe ni kurekebisha vifungu vinavyohusiana na uchaguzi ndani ya Katiba. Maana tatizo sio Katiba, Bali tatizo ni mfumo danganyifu(Nyoka wa Kijani)
18. Msifanye Siasa kwa mazoea na kuogopa vitisho vya kijinga. Ni heri kufa kuliko kuogopa Kitisho. Badilikeni kila wakati.
19. Msivae mavazi yenye mfumo wa Kombati kwa kipindi hiki kwa kuwa huo ni mfumo wa Harakati. Twende na mfumo mpya wa Uongozi. Tukubali kubadilika.
20. Mungu apewe nafasi ya kwanza kabla ya yote katika shughuli zenu. Piga chini Kamati zote za Ufundi ndizo zinazo waangusha sana.
NB: Nimeamua kuishia hapa na 10 zilizo bakia mtanitafuta manually kwa wakati wenu ili tuzimalizie zilizobakia. Nawapenda sana.
NJIA YA 21-23 YA KUIPOROMOSHA CCM 2020.
Rafiki yangu mmoja kaniambia niongeze tatu, nami naongeza:
21. Vyama vyote vya Upinzani kuna ulazima kurekebisha mfumo wenu wa muungano, mfumo uliopo sasa umeangalia zaidi vyama vyenye wabunge au ushawishi ambao ndio UKAWA. Sasa basi mfumo ubadilike na kujumuisha vyama vyote vya Upinzani vyenye wabunge, vyenye ushawishi na vyama vyenye Wenyeviti Makini lakini havina wabunge wala madiwani. Uunganiko hili litaleta radha ya matumaini yajayo ya Ushindi kutokana na kuingiza watu wazoefu na wakongwe wa siasa za Upinzani kutoka mwaka 1992 yaani tangu mfumo wa vyama Vingi uingie nchini.
22. Baada ya kuaandaa mgombea Urais na kupatikana, kinachofuata sasa ni wale wenye viti wote wa vyama vidogo wapewe majimbo ya kugombea Ubunge 2020 bila kujali ushawishi wa chama. Kwani kwa kufanya hivyo Mungu anafungua milango kwa wale tulio wasahau. Huwezi ukamuacha nje Kuga au Rungwe au Dovutwa wakati ni wakongwe mhimu wa siasa. Tujifunze kupambanua na tuweke chuki pembeni ili tushinde sekta zote.
23. Mgombea Urais aanze kuandaliwa bado mapema. Mnapashwa kuandaa watu watatu ambao mmoja wao ndio atawakilisha. Katika hao mlengwa afahamike na wengine wawe ni Emergence. Mgombea aandaliwe kwa Umakini sana na kwa siri kidogo.
Nawatakia kazi njema ila sasa 7 zilizo bakia tuonane kiofisi.
NJIA 24-25 YA UPINZANI KUIANGUSHA CCM 2020.
Nimeona ni fahari kuwasaidieni hata mkinikejeli lakini mtanikumbuka:
24. Sera sadifu, hakikisheni mnakuwa na Sera za aina mbili, Sera itakayotumika kuongoza nchi na Sera itakayotumika kulingana na uhitaji. Linganisheni Sera za mataifa mbalimbali na Taifa letu na kuona ni wapi pa Ku copy na Ku paste na wapi si pakuchukua kabisa. Hii itasaidia kuanza kujijenga kuongoza Dolla 2020.
25. Tathimini na Ukosoaji; kila mnapo maliza mkutano au kikao, viongozi sharti mkubali kukusolewa hata kama mjumbe atawakera au kuwakasirisha lakini msichukie. Maana katika kukosoana ndipo tunajua ni wapi tumejikwaa. Kwa kufanya hivi tutazidi kupata mbinu nyingi za kukamata dolla.
Zimebaki 5, inatosha sana.
NJIA 26 YA UPINZANI KUING'OA CCM 2020.
26. Zanzibari iandaliwe wagombea ambao ni watu mashuhuri na wenye nguvu ya ushawishi. Ambao watasababisha ushindi mkubwa. Kulingana na mazingira ya Zanzibar kwa nafasi ya Urais si kila mtu anastahili Bali mvuto na ushawishi, unajua ubabe sio ushawishi Bali ni kukosa mvuto.
Hivyo lazima tuangalie MTU sahihi wa kuibeba Zanzibari yetu.
Nimewaongezea fursa ingine hiyo.
NJIA 27 UPINZANI KUIPOROMOSHA CCM 2020.
Nawafariji kwa hili pia;
27. Serikali ya Mseto kabla ya 2020, ikitokea mkaamua kuunda SERIKALI ya mseto kabla ya 2020 kuweni makini sana, maana ndio njia zilizo wamaliza Maalim Seif, Shangilai na Odinga. Mnapoingia katika Mseto msikubali kuwadhalilisha watu wasio na hatia itakuwa ndio mtego kwenu. Msiingie kwenye mitego ya rushwa na deal za magumashi. Fanyeni kazi hasa bila kuchoka mpaka wasahaulike na kujuta kuwapa Mseto. Wakiwapunguza nguvu mnajivua madaraka ili kulinda heshima yenu. Kwa kufanya hivyo 2020 njia ni nyeupe.
Msiogope vikwazo na mapingamizi hata Mimi Deogratius Kisandu naumia na udhalilishaji na vikwazo nilivyowekewa. Pigeni kazi, Mungu atawafanikisheni.
Mchana mwema;
NJIA YA 28 YA UPINZANI KUIANGUSHA CCM 2020.
Mbinu hii ya nyongeza;
28. Ushindi upo mezani. Issue siyo kufanya mikutano mingi, hapa mnatakiwa kukaa na kupanga mikakati ya kushinda iwe kwa kuiba kura au kupora masanduku ya kura au kutumia mawakala wakuu vizuri au kucheza na tume vizuri au kukaa na wadau vizuri au kujua karatasi za kupigia kura zinatokea wapi au eneo la uchaguzi likoje kiushindi au mentality ya wananchi ikoje kwa chama chenu au kuinua watu wenu wote wenye vipaji halisia n.k
Lazima kuwa na mikakati inayotembea bila woga, kujengana kiimani juu ya ushindi. Chaguzi ndogo msibweteke na umati wa watu maana eneo ni dogo lakini watu waliokuja mkutanoni ni wengi lakini wapiga kura ni wachache kati yao. Tembeleeni wapiga kura kabla ya mikutano NYUMBA kwa NYUMBA.
Deogratius N Kisandu
10 Januari 2017