Enyi wanaume ishini na wake zenu kwa akili

satong

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
260
311
C & P
________________________________________
Unaweza kumpigia simu mpenzi wako mkale bata mahali flani akakwambia hana nauli na wakati anakipato kizuri tu na mbaya zaidi nauli haizidi hata buku, lakini anaweza kuja na bajaji wakakupiga buku 15. Halafu bili ikija hawezi kulipia hata maji ya kunywa, unaumilia moyoni utadhani umekula peke yako. Hapo ndipo utaelewa kwa nini Biblia inasema,“Enyi wanaume ishini na wake zenu kwa akili". Kama huna akili wallahi mwanamke atakushinda, na kumbuka akikushinda utabaki kuwatukana wanawake wote kwamba ni kunguru. Yaani usivyo na akili unasahau kwamba hata mama yako ni mwanamke! Nakwambia kama uko kwenye mahusiano na ukashindwa kutumia akili usipojinyonga basi utanyonga. Mke na mume walihudhuria semina ya ndoa. Mada ilikuwa namna ya kunogesha unyumba na mwezeshaji alifundisha kwa mbwembwe mpaka raha. Anakwambia mwanamke anakamatwa hivi, mara vile, mara sijui nini. Basi katika hali ya utani, mke akamgeukia mumewe na kuuliza,“Utayaweza hayo hubby? Mume aliinuka kwa hasira akamkamata umma na kumchoma mkwe wake kichwani na kufa pale pale. Mume alikosa akili.

Labda nikwambie mwanaume mwenzangu, kuishi na mwanamke ni sanaa wala siyo sayansi ndio maana wahenga wanasema “mwanamke nywele”. Mitindo mbali mbali ya nywele za wanawake ni ujumbe kwetu wanaume kwamba wanawake wanahitaji utofauti. Hawataki mazoea. Sasa wewe kariri tu kwamba mke anapigwa kwa vitenge, utanunua vitenge vyote vya Congo na bado akakuona zombi tu. Mazoea huleta dharau. Unajidanganya kwamba pesa kwa mwanamke ni kila kitu, na kweli unammwagia pesa, mwisho wa siku pesa zako zitaliwa na konda.Konda anakula pesa zako kwa sababu ya ubunifu alionao. Yaani konda ana akili kukushinda? Acha ujuha bro, mwanamke hahitaji pesa, anahitaji uniqueness. Hataki mazoea, anataka ubunifu kama anavyofanya kupitia nywele zake. Leo nywele ataweka hivi, kesho zitarefuka kama mkia wa jogoo, mara atazilaza usoni na kufunika jicho, yuko tayari jicho lisione siku nzima ilimradi aonekane unique siku hiyo. Unaweza kusema ni ujinga kumbe ndo walivyoumbwa. Haya mambo hayahitaji PhD kuyaelewa. Ni kucheza na akili tu. Shauri lako.

Wengine wanajidanganya kwamba mwanamke anahitaji umpe muda wa kukaa naye, hataki mwanaume aliye busy. Hivi kuna mtu busy kama konda? Kuna mtu busy kama house boy? Kuna mtu busy kama derevea wa bodaboda? Kuna mtu busy kama maskini wa Afrika? Maskini wa Afrika anafanya sana kazi kwa malipo kidogo. Kwa taarifa yako hao ndio wanaokula pesa zako? Labda nikuibie siri tu. Mwanamke anapenda sana kusikilizwa. Ni mtu anayependa kusema anayowaza, aliyoona au kukutana nayo. Furaha yake ni kusema. Muache akusimulie yote aliyokutana nayo mchana kutwa. Sasa akiona humsikilizi atafikiri hampendi na kuamua kutafuta wa kumuelezea. Sasa akiangukia mikononi mwa mwanaume anayejua kusikiliza basi ujue mke hunaye tena. Jiandae kulea watoto wa mume mwenzako kwa jina lako. Ndo maana unaweza kuta mke wa tajiri anatembea na mfagia choo cha soko madamu tu anajua kusikiliza. Ishini na wake zenu kwa akili.

Mke wako anahitaji kusifiwa yeye tu. Usijaribu kumsifia mwanamke mwingine mbele ya mpenzi wako, hata kama ni kwenye picha au televisheni wewe ziue. We sifia uzuri wake, umbile lake, macho yeke, nywele zake, shingo yake, hipsi zake, msifie alivyomechisha nguo zake na kipochi, mkufu, hereni ,viatu, saa na cover ya simu. Kila wakati ukimuona mwambie amewashinda wote. Usipomsifu hatapenda kuwa karibu na wewe, atapenda kuwa karibu na wanaomsifia. Muache alale kifuani kwako kwa sababu hutamani kuguswaguswa na kupigwa busu. Kasheshe kama anakuzidi uzito ndo utaipata, lakini usijali mtengenezee bembea. Nilikuwa nachomekea tu.
Yanatosha kwa leo.
 
Usiwachukulie serious sana Mkuu..ni living nuclear! Ni mama zetu lakini dah..
 
umewadharau sana makonda aisee...
yaani wao hawana akili??
 
Haya tumesikia

Yanatosha kwa leo.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom