Kuna mambo yanayotokea kwenye nchi yetu tunayadharau na kusema hayatuhusu. Azori katoweka hayatuhusu, Lissu kapigwa risasi hayatuhusu, Lema kakimbilia kenya hayatuhusu, matokeo ya uchaguzi yana utata hayatuhusu, uhuru wa vyombo vya habari umeminywa hayatuhusu, mwishoni itakuwa kama ile hadithi ya panya.
Ng'ombe na mbuzi wanachinjwa kisa walidharau taharifa ya panya kuwa kuna nyoka aliyeko uvunguni mwa kitanda.
Kinapokuja kibano kinatuhusu wote bila kujali chama, dini, kabila mf kufungiwa intanet ilituhusu wote.