Engineer Anatafuta Kazi

jerrto

Member
Joined
Feb 25, 2014
Posts
46
Reaction score
15
Wandugu kama kuna mtu ana kampuni au anafahamu kampuni yoyote ambayo inatafuta Electrical Engineer, tujuzane maana maisha ya hapa mjini yanakaza kuliko maelezo.
 
Wandugu kama kuna mtu ana kampuni au anafahamu kampuni yoyote ambayo inatafuta Electrical Engineer, tujuzane maana maisha ya hapa mjini yanakaza kuliko maelezo.
MAINJIA wa Tanzania bwana, kipindi nasoma pale mlimani kuna mwaka hao vijana wanaosoma engineering walitengeneza gari walipoliwasha likawa linarudi nyuma kwenda mbele halitaki.......... hahahha
 
Am also electrical engineer kaka nashangaa unatuabisha bro mbona kazi zetu ziko nying sana umemaliza chuo gani mkuu na mwaka gani then mtajua jinsi ya kukusaidia na mtajua wapi unapokosea
 
Am also electrical engineer kaka nashangaa unatuabisha bro mbona kazi zetu ziko nying sana umemaliza chuo gani mkuu na mwaka gani then mtajua jinsi ya kukusaidia na mtajua wapi unapokosea
UDSM kaka,sema nipo kampuni moja ya consultancy wanatoa hela njiwa sana so nafikiria kuhusu contractors kidogo si unajua kule hela za site kibao,huku mshahara tu hata site hatuendi so life linakaza kihivyo
 
Hapo nimekuelewa, vinginevyo nilitaka kushangaa kwamba huna kaz kabisa.
 
Wandugu kama kuna mtu ana kampuni au anafahamu kampuni yoyote ambayo inatafuta Electrical Engineer, tujuzane maana maisha ya hapa mjini yanakaza kuliko maelezo.
Unaweza kazi za kwenye minala ya simu..??

Am also electrical engineer kaka nashangaa unatuabisha bro mbona kazi zetu ziko nying sana umemaliza chuo gani mkuu na mwaka gani then mtajua jinsi ya kukusaidia na mtajua wapi unapokosea

UDSM kaka,sema nipo kampuni moja ya consultancy wanatoa hela njiwa sana so nafikiria kuhusu contractors kidogo si unajua kule hela za site kibao,huku mshahara tu hata site hatuendi so life linakaza kihivyo

Bado hujasema umemaliza lini?Hiyo kampuni ya consultancy uko nayo kwa muda gani hadi sasa?
 
almost eight months!does it matter???
so umemaliza chuo mwaka jana..? 2013 sio ..?
najua kwa hizo consultancy firm wana-UNDER pay sana simply sababu wanayotoa ni upatikanaji wa kazi kwa manati.. sababu nyingine wanayosema huna experience wanakufundisha kazi vilevile wanakusupervise kuelekea kuwa registered engineer professional..(ukiweza vumilia hapo japo kidogo upate japo mradi mmoja tu usupervise then utafute chaka)..
kazi za UMEME ni nyingi sana KANUNI ya kwanza ambayo naweza kukushauri pokea kiasi kuanzia 500-800 kwa kuanzia kama wewe ni graduate lakini kama u-makini na uko FOCUS unajua unachotaka kufanya ndani ya mwaka mmoja thamani yako (VALUE) inapanda maradufu mathalani viwanda kama ALAF, na viwanda vingi vya wahindi wanalipa watu chini sana
ila sasa ukikaa nao hawa jamaa zikitoka nafasi kama TWIGA,TPC, TCC,TBL uwezekano wa wewe kupata kazi ni mkubwa sana kuliko freshers(yule anayetoka shule simply unaconsiderable experience tofauti na huyo fresher na uko kwenye position nzuri ya kubargain salary ambayo walau itakutoa point A na kukupeleka point B..) moja ya tatizo kubwa sana ambalo vijana wengi tunashindwa ni uvumilivu NAJUA maisha ni magumu na unakuwa na majukumu mengi na MATARAJIO mengi mno..
kwa umeme kuna kampuni nyingi sana za ukandarasi ambazo kama uko vizuri unaweza jifunza mambo pia na wewe ukafungua kampuni yako fursa ni nyingi sana ni UJASIRI tu...

pia jitahidi kuomba kazi sehemu nyingi na unaweza kwenda ana kwa ana kwenye ofisi hizi mfano NAMIS, MOLLEL, INTERCITY, DERMS ELECTRIC ,UR, ,TANESCO, ukapeleka CV zako hata kama awajatangaza kazi wengi huwa hawatangazi kazi so unaweza kuwa na bahati yako...

najua wazee wa consultancy na wahandisi wengi wako vizuri professional na wanapata miradi mingi na wengi ndio wanaijua shughuli hii ilivyo muhimu ila sijui kwanini wanalipa watu hela ndogo sana..
ERB na wajua mtiti wa uhandisi ila kutetea maslahi ndio shida

YOTE KWA YOTE USIKATE TAMAA UJAKOSEA KOZI NAJIVUNIA SANA HII KOZI .. NAIPENDA SANA NA FURAHIA INGAWA BADO MATUNDA YA FINANCIAL REWARDS BADO NAAMINI ITAPATIKANA TU ..
 
MAINJIA wa Tanzania bwana, kipindi nasoma pale mlimani kuna mwaka hao vijana wanaosoma engineering walitengeneza gari walipoliwasha likawa linarudi nyuma kwenda mbele halitaki.......... hahahha

kinachochekesha hapo ni kipi sasa?

kama ulikuwa unajua chochote si ungeenda basi?
 
almost eight months!does it matter???
Maganga Mkweli kamaliza,fuata vizuri ushauri wake!Miezi minane ni kidogo sana,kijana acha tamaa,mbuyu ulianza kama mchicha!Mshukuru Mungu kwamba una kazi katika consultancy firms,ni sehemu pekee ambayo unaweza kujifunza kazi na ukiweza kukaa miaka 2 tu basi utaweza kufanya kazi mahali popote hata ukitaka kujiajili!Cha msingi ndani ya hiyo miaka 2 hakikisha unafanya mipango unaanza SEAP na unakamilisha usajili wa wahandisi ERB!Watu wanatafuta hata wafanye kazi bure kwenye consultancy firms ili waweze kujua kazi!Kuwa na subira kijana,uko mahali sahihi kabisa,chapa kazi!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…