Kazi ipo kweli kweli miaka si mingi iliyopita ulikuwa mtu uki taja shillingi 100.00 nicknamed masai watu wanakuogopa, baadae ikawa elfu, ikafuatiwa na laki, miaka ya hivi karibuni tumeambiwa laki si pesa, kumbe hata millioni inaanza kukosa umaarufu, sasa tunaongelea billioni, yaani ukisikia mtu kafisadi au kalipwa tenda ni mabillioni, hata nyumba ya kawaida sana isiyo ya gorofa na kiwanja chake ni biliioni? hii nchi inaenda wapi?? Kuna haja ya kuongeza maombi. Fikiria nchi kama UK pamoja na kwamba wao waliaanza haya maisha ya kisasa karne nyingi sana kabla ya sisi hatujaamka lakini noti kubwa ya pesa yao ni 50, tena hilo noti la 50 halipo kwenye mzunguko wa biashara za kila siku, noti kubwa la kwenye matumizi ya kawaida ni 20, sisi tuna manoti mpaka 10000 na bilioni ndo pato la kawaida la kufanyia biashara???? watanzania tumelogwa, nasema tena tunahitaji maombi