Endeleeni ku-fake mambo

Endeleeni ku-fake mambo

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Kwahiyo baada ya uongo na maisha yote ya maigizo acheni ukweli angalau upewe nafasi. Sababu dunia hii ya maigizo na sifa nyingi zenye kuwafurahisha watu, ndio inatufanya tuishi kwa kushindana na kutaka kujionesha nani ni bora na nani ni dhaifu.

Maisha ya maigizo na ku fake uhalisia wa hali zetu ndio unafanya binadamu wakae chini kuwaonea wivu watu ambao walitakiwa kuonewa huruma.

Mitandao ya kijamii ndiyo inafanya binadamu wafikie hatua ya kumkosoa Mungu, nasikitika kuongea hilo sababu wengine wameenda mbali sana kuamua kuingia gharama kujitengeneza miili yao ili wawavutie zaidi watu wengine.

Hii ndio dunia yetu ya sifa na pongezi, dunia ambayo huwezi shangaa kumuona mdada aliye kwenye ndoa akijitahidi sana kupiga picha za utupu ili tu asifiwe na wanaume wengine kwenye social media.

Eeenh! ni dunia yetu, dunia ambayo kusema ukweli ni kosa ila kumsifia mtu kwa uongo ni fursa.

Aaaaaanh! Karibu ujionee dunia hii ya uongo na kweli, dunia ambayo watu wanajikataa jinsi walivyo sababu ya mionekano ya uongo ya watu wengine.

Leo hii watu wanajitambilisha na kujidhihirisha mbele ya watu wengine kwa maisha ambayo wao wenyewe hawajawahi kuyaishi wala hawayajui. Hivi sasa uongo umekuwa ni dili sana kiasi kwamba msema ukweli anaonekana ni mwenye hatia.

Dunia ya Facebook, dunia ya Instagram, dunia ya WhatsApp na TikTok, ndio dunia ya nusu uchi, dunia ya ushoga na usagaji dunia ya dhambi za wazi.
Na ndio hii hii dunia ya Twitter, dunia ya "watoto washalala threads".

Lakini kila mnapojitahidi kudanganya msisahau kukumbuka kuna maisha baada ya uongo, kuna maisha baada ya hayo mnayoyafanya. Jifunzeni kuishi maisha halisi, ili yawe rahisi, msipate ukakasi mkapitiwa na Ibilisi mkaja kuasi dhambi zikawawaka mithili ya nyasi.

Acheni kutafuta attention kwa watu, hizo likes, comment na shares mnazozisaka kwa udi na uvumba hazina maana yoyote ile kwenye maisha yenu halisia. Sababu hata shida zitakapokujia, hazitaweza kukusaidia.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza, wenu katika kalamu Amani Dimile

IMG_20231019_193111_909.jpg
 
wanajikataa jinsi walivyo sababu ya mionekano ya uongo ya watu wengine.
hahaa ukiwa mbaya utajijua tu na itakua ngumu kujikubali,

na hata hivyo sio mitandao ya kijamii tu ndo inahukumu watu kwa mionekano, hali hii ilikuwepo tokea zamani ndo binadamu walivyo.... mfano mtoto mnene lazima ataonewa na wenzake, watoto wanatumia mitandao?

enewei, dunia haina huruma
 
A
Kwahiyo baada ya uongo na maisha yote ya maigizo acheni ukweli angalau upewe nafasi. Sababu dunia hii ya maigizo na sifa nyingi zenye kuwafurahisha watu, ndio inatufanya tuishi kwa kushindana na kutaka kujionesha nani ni bora na nani ni dhaifu.

Maisha ya maigizo na ku fake uhalisia wa hali zetu ndio unafanya binadamu wakae chini kuwaonea wivu watu ambao walitakiwa kuonewa huruma.

Mitandao ya kijamii ndiyo inafanya binadamu wafikie hatua ya kumkosoa Mungu, nasikitika kuongea hilo sababu wengine wameenda mbali sana kuamua kuingia gharama kujitengeneza miili yao ili wawavutie zaidi watu wengine.

Hii ndio dunia yetu ya sifa na pongezi, dunia ambayo huwezi shangaa kumuona mdada aliye kwenye ndoa akijitahidi sana kupiga picha za utupu ili tu asifiwe na wanaume wengine kwenye social media.

Eeenh! ni dunia yetu, dunia ambayo kusema ukweli ni kosa ila kumsifia mtu kwa uongo ni fursa.

Aaaaaanh! Karibu ujionee dunia hii ya uongo na kweli, dunia ambayo watu wanajikataa jinsi walivyo sababu ya mionekano ya uongo ya watu wengine.

Leo hii watu wanajitambilisha na kujidhihirisha mbele ya watu wengine kwa maisha ambayo wao wenyewe hawajawahi kuyaishi wala hawayajui. Hivi sasa uongo umekuwa ni dili sana kiasi kwamba msema ukweli anaonekana ni mwenye hatia.

Dunia ya Facebook, dunia ya Instagram, dunia ya WhatsApp na TikTok, ndio dunia ya nusu uchi, dunia ya ushoga na usagaji dunia ya dhambi za wazi.
Na ndio hii hii dunia ya Twitter, dunia ya "watoto washalala threads".

Lakini kila mnapojitahidi kudanganya msisahau kukumbuka kuna maisha baada ya uongo, kuna maisha baada ya hayo mnayoyafanya. Jifunzeni kuishi maisha halisi, ili yawe rahisi, msipate ukakasi mkapitiwa na Ibilisi mkaja kuasi dhambi zikawawaka mithili ya nyasi.

Acheni kutafuta attention kwa watu, hizo likes, comment na shares mnazozisaka kwa udi na uvumba hazina maana yoyote ile kwenye maisha yenu halisia. Sababu hata shida zitakapokujia, hazitaweza kukusaidia.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza, wenu katika kalamu Amani Dimile

View attachment 2786627
Aisee,afadhali wewe umeyajua!
 
Back
Top Bottom