Embe cherema laoza

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,405
EMBE CHEREMA LAOZA.







1)umepata mkataji,mti pale ulikwepo.
Wakaufanya mtaji,virukaruka vipopo.
Waze wakuda wa jiji,wafa kuitwa makopo.
Embe dodo licherema,laiza likilalama.







2)embe leo mfamaji,acha lizame mi sipo.
Limepata mnyoaji,hatari hapo ilipo.
Lataka jifanya jaji,kwa uchawi ungalipo
Embe dodo licherema,laoza likilalama.





3)kisa lilikosa shamba,embe lafungua domo.
Dodo liache ushamba,ugali upi kikomo.
Wote wataka kutamba,na kuchuma kila chumo.
Embe dodo licherema,laoza likilalama.






4)dodo lanyaa magamba,lisitutishe ngurumo.
Sura yake ni ya pamba,tumeshapima kipimo.
Tulipigishe jaramba,likazame kwenye shimo.
Embe dodo licherema,laoza likilalama





Shairi:EMBE CHEREMA LAOZA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.



0765382376.
 
Back
Top Bottom