lukesam
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 12,444
- 25,710
Mimi sina tatizo na wao kupata msamaha, kwasababu mamlaka ya rais katika kutoa msamaha hayahojiwi!Magu akiwa kwenye kutafuta sifa na kick za kijinga huwa haoni aibu. Hilo la Babu Seya nimeharibu kabisa taswira ya kitaifa katika vita dhidi ya ubakaji.
Watu waliotiwa hatiani na mahakama kwa makosa ya ubakaji sio watu wa kujipendekeza nao hadharani.
Those people can easy spoil your image.
Tatizo langu ni pale wabakaji na walawiti(kwa mujibu wa mahakama zetu tukufu) wanapopata msamaha wa rais na kuonekana kama mashujaa wa vita ya pili ya dunia, kukaribishwa ikulu pamoja na kupata heshima kubwa kutoka kwa viongozi wa serikali kama Naibu waziri..
Tumefika mahali kweli wabakaji waliosamehewa adhabu(sio kufutiwa kosa) wanaonekana kama mashujaa waliotoka vitani?
Tunakataza waliopata mimba wasirejee shuleni bila kujali walipataje hizo mimba,wakati huo huo tunawapatia wabakaji heshima ya kutukuka!