Elon Musk anakuja Kuiteka Dunia

Elon Musk anakuja Kuiteka Dunia

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
830
Reaction score
902
BAADA YA SPACE X NA X CORP,NI ZAMU YA NEURALINK:
Bilionea Elon Musk amefanikiwa kubadili jina la mtandao wa twitter kuwa X Corp,akaliondoa lile alama yao ya njiwa akapachika alama yake ya X.Hii ni baada ya kununua twitter.

Pesa kweli inaweza kuvunja mlima,nimeona hata mlima ule maarufu wa Ukonga unatoweka

Na sasa bilionea namba moja huyo ulimwenguni ameamua kwenda mbali zaidi. Elon Musk, kupitia kampuni yake ya ''Neuralink'' sasa wanatafuta watu ambao watakuwa tayari kujitolea ili kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwa ajili ya kupandikizwa ''chip'' kwenye ubongo.

Mfumo huu wa ''Neuralink'' unahusisha kuondoa kipande kidogo cha fuvu kwenye kichwa cha mgonjwa aliyekumbwa na maradhi ya kiharusi, na kupachika mfumo huu kupitia kifaa maalumu ili kusudi kimsaidie kurejesha hali ya uwezo wa kufikiri kama kompyuta.

Ijapokuwa kwa wagonjwa wa kiharusi kwa sasa wanatumia mfumo wa ''brain-computer interface (BCI)'' ambao unaunganishwa na fuvu la kichwa kwa msaada wa Akili mnemba (A.I) ambao unamuwezesha mgonjwa kuwasilisha mawazo yake kwa mfumo wa sauti.

Na mfumo huu kwa sasa unamuwezesha mgonjwa kuzungumza maneno 78 kwa muda wa dakika moja, lakini wanapanga kufanyia maboresho kumuwezesha mgonjwa kuzungumza maeneno 150 kwa lisaa.

Bado haijafahamika kama mfumo wa ''Neuralink'' utaweza kumsaidia mgonjwa zaidi ya mfumo huu wa Akili mnemba kupitia (BCI) pengine tusubiri matokeo ya majaribio yatasema nini kuhusu mfumo huu.

Kwa mujibu wa wavuti wa Fox,kuna masharti machache kwa watu wanaohitajika kwa ajili ya kujaribiwa kwenye mfumo huu wa ''Neuralink'':

1. Wawe chini ya umri wa miaka 40.
2. Wawe wenye kusumbuliwa na kiharusi.
3. Wawe tayari kwajili ya hayo majaribio.

Sipingi sana hili kwa sababu nia ni njema,ila naogopa tunakoelekea kwa sasa.Huu mfumo wa AI unaokuja kwa kasi katika kila sekta unamadhara makubwa,baadaye.

Nini maoni yako?elo
 
Mtu akipandikizwa hiyo anaweza kuongea lugha yoyote ile ,sasa mtu akiwa na mfumo huo anaweza kutafuta material kama computer.

Mtu huyo akiingia kweny chumba cha mtihani itakuwaje!?Kiufupi hata mitihani haitakuwa ishu tena
Mitiani ni mbinu ya kugawana Ajira na kodi tu kila kitu kinahitaji kujifunza na sio mitihani ya shule unaweza ukawa na masters lakini usijue kutumia computer au kuendesha gari lazima ujifunze.
 
Kwa ujumla huo ndio ule ulimwengu wa kishetani kutawala dunia tuliohubiriwa kuna nyakati utakuja. Hapa habari za Mungu hazitahubiriwa, itakuwa ni ulimwengu wa akili mnemba tu kwa kila kitu
 
Mtu akipandikizwa hiyo anaweza kuongea lugha yoyote ile ,sasa mtu akiwa na mfumo huo anaweza kutafuta material kama computer.

Mtu huyo akiingia kweny chumba cha mtihani itakuwaje!?Kiufupi hata mitihani haitakuwa ishu tena
mtihani wa nini wakati yeye mwenyewe mtihani
 
Back
Top Bottom