ELIMU YETU

Chipukizi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
4,643
Reaction score
7,120
Nimeiona pahali Fulani Nini Maoni Yako mwana JF??

ELIMU YETU
Leo tumeanza mitihani hapa chuoni. Kitu kimoja kuhusu elimu ya Tanzania kinanijua akilini wakati naamka kuwahi saa 12 niwe ofisini. Elimu ya Tanzania ni kama mzazi asiyejua amleeje mwanaye. Wakati mzazi huyo anamlaumu mtoto, na mtoto naye hamwelewi baba. Elimu ya Tanzania ni kuwa mwalimu anajua anachotakiwa kufundisha, lakini hajui kwanini anafundisha, hivyo hajui lengo kama limetumia au hapana. Na hivyo hajui pia kama abadilishe cha kufundisha sababu lengo limetimia au abadilishe namna ya kufundisha sababu lengo halitimii kama alivyotaka.

Elimu ya Tanzania ni mzazi ambaye anamwangalia baba wa jirani anavyolea wanawe na anaiga bila kujua kwanini mwenzake analea wanawe anavyofanya and to what end. Yaani ni sawa na baba mwenye mradi wa kukodisha maguta, na jirani yake ana mradi wa kukodisha malori. Wanakutana wanapiga stori, baba wa malori anamwambia baba wa maguta kuwa amempeleka mwanaye driving school. Baba wa maguta akirudi nyumbani naye anamchukua mwanaye driving school. Baada ya miaka wanakutana tena, baba wa malori anamwambia kuwa amempeleka mwanaye kujifunza utengenezaji wa malori. Baba maguta anarudi nyumbani anamchukua mwanaye kujifunza utengenezaji wa malori.

Yaani elimu yetu ni elimu isiyoangalia tunahitaji nini na hivyo tufundishe nini. Na tukishafundisha tutajuaje kuwa lengo la mahitaji yetu limekamilika na sasa tuna hitaji jipi jipya na hivyo tubadilishe tunachofundisha. Sisi ni kama baba wa maguta, tunapeleka watoto driving school sababu tumemuona baba wa magari kapeleka wanawe, bila ya kufikiri kuwa hatuna gari, sisi tunatakiwa tupeleke watoto wetu shule ya kusukuma guta. Kesho tunampeleka kutengeneza magari wakati hatuna magari tulitakiwa tumpeleke shule ya kutengeneza na kukarabati maguta. Sisi tutaanza leo na mtaala wa kilimo, kesho tunasikia Ulaya na Marekani wana gender, tunaacha kilimo tunakwenda kwenye gender. Baada ya wiki tunasikia kuna globalisation tunaacha kujifunza namna ya kutafuta maji ardhini maana watu wetu hawana maji tunaingiza globalisation. Baada ya mwaka tunasikia kuna climate change, tunaacha vyote tunachangamkia climate change. Baada ya miaka miwili tunasikia kuna AI, tunaacha tena tunaingia kwenye AI. Elimu yetu ni ya kurukia kila kitu and master of none. Yaani wenzetu wana-master kilimo, wakienda kwenye lingine ni kuwa hitaji la kilimo wamelitatua. Sisi tunahama hata hatujui tuna hitaji gani na tutapata nini katika hilo tunalohamia. Sisi tunatia huruma, na ndo maana elimu yetu haisaidii si sisi wenyewe wala jamii yetu kwa ujumla. Mbaya zaidi ni kuwa kadiri siku zinavyokwenda wanaojua haya matatizo ninayoongea wanazidi kufariki na wanaokuja ni hao wasiojua na ndo taratibu wako kwenye maamuzi ya mustakabali wa taifa. Hao hawajui kwa nini tunafanya tunachofanya; wao ni kila kitu Ulaya wanafanya, Marekani wanafanya… Sisi tumekuwa kama ngedele kila tukishikwa mkia tunageukia huko tulikoshikwa. Hatuja-master hata basic ya kutengeneza gari la injini tumeona wenzetu wanahamia kwenye electric cars, na sisi tumo tumehama. Hatujatengeneza hata computer au hata program ya kuendesha computer, tumehamia AI.

Sisi ni vichaa tusiojitambua. Ni kama mtu mwenye njaa hana chakula hata kidogo sababu hazalishi chakula cha kutosha, anakaribia kufa yeye na familia yake, anapata hela anakwenda kujifunza jinsi ya kula chakula badala ya jinsi ya kuzalisha chakula cha kutosha, sababu tu kamuona jirani yake anasomea jinsi ya kula. Lakini hawezi kutambua kuwa jirani yake hana shida ya uzalishaji. Unasomeaje kula na huna hicho chakula? Elimu yetu ina shida kubwa lakini hakuna anayekubali maana wengi wetu ni malimbukeni wa kununua kila iphone mpya inayotoka, hata hatujui ina nini kipya na mahitaji yangu yanahitaji hicho kipya. Kwenye iPhone mpya. Maisha yetu ya kawaida haya ya iPhone na Samsung yana-reflect akili ya jamii yetu na mwisho elimu yetu. Kama taifa tuna tatizo, kama jamii tuna tatizo, elimu yetu ina tatizo na anguko lake ni kuu sana.
Shuck (udsm, 3 March 2026)
 
Elimu ni bidhaa

Unachohitaji ndicho unachopaswa ukizingatia kwa kukinunua

Ukiwa mpumbavu kila kitu utahitaji

Hakuna mwisho wa Elimu kama ilivyo hakuna mwisho wa mahitaji na tamaa za Binadamu

Maana yake ikiwa bado vita yako ni afya somesha wahasibu kwa uchache lakini nguvu nyingi ukielekeza kwa matabibu kwa asilimia kubwa

Kwa TZ watu bado wananjaa keria ya Agricultural inabambaa zaidi kuliko Aviation

Pata unachohitaji kwenye elimu na siyo kupika makande na mapilau kulazimisha kupata ladha zote kwenye chakula kimoja japo inawezekana ila si wote wanamudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…