TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,674
- 1,572
Jana baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo katika matokeo hayo ufaulu umeonekana kushuka kwa zaidi ya asilimia moja.
Pia katika matokeo hayo, hakuna shule yoyote ya serikali iliyoingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri.
Najua watakuja na sababu nyingi, watatueleza mengi zaidi. Kinachonikera mimi ni kuukwepa ukweli na kutoa sababu ambazo hata wao wanajua kwamba ni uongo.
Watatuambia labda ni mabadiliko ya mfumo wa utunuku wa alama, uchache wa walimu w sayansi nk.
Ukweli ni kwamba walimu wa taifa hili wamesuswa, walimu wa taifa hili wanamigomo yao ya rohoni, wanafanya kazi wakiwa na vinyongo vingi moyoni.
Mwalimu wa diploma anayeanza kazi anaanza na Mshahara TGTSC ambapo ni shilingi 532,000 (basic salary) ambapo baada ya makato mwalimu anapata 430,000.
Mwalimu wa ngazi ya cheti (primary school) anaanza na TGTSB ambapo ni sawa na 389,000 (basic salary) ambapo baada ya makato anapata 287,000.
Hii ni mifano tu, kwa hali hiyo mwalimu anaishi vipi. Mwalimu anatakiwa alipie nyumba, usafiri, nk.
Tuache kuzunguka, iwapo serikali ya CCM, wanataka kuinua kiwango cha elimu basi tujali walimu kwanza.
Tutoe hata teaching allowance kila mwezi kwa walimu walau laki mbili kwa kila mwezi.