Nikiangalia kipindi cha minibuzz, watu wanafikiri elimu ya uraia, haki ya kupiga kura itasaidia kuwezesha kupata viongozi bora.
Mimi naungana na mshiriki mmoja ambaye kwake kupiga kura si jambo muhimu.
Kiukweli kama hakuna mfumo wa kuwadhibiti na kuwawajibisha viongozi wetu wawapo madarakani na baada ya kipindi chao cha uongozi, tusitegemee kupata maendeleo na kuweza kujipambanua dhidi ya maadui wetu kama maradhi, umaskini na rushwa.
Maana ya uongozi imeshabadilishwa, badala ya kutumikia, sasa ni kutumia.
Nionavyo mimi tunachohitaji ni jinsi gani viongozi wetu tunawawajibisha baada ya kuwaweka madarakani, hiyo itasaidia kuwadhibiti dhidi ya ufisadi na kutowajibika.