Elimu ya tanzania na mustakbali wa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya tanzania na mustakbali wa taifa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mzamifu, Aug 28, 2012.

 1. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Wakati wa ukoloni elimu ilikuwa ikitolewa kwa matabaka kwa kuzingatia rangi na hata dini. Tulipopata uhuru muasisi wa taifa letu mwalimu Nyerere alitaifisha shule zote zilizokuwa zikiendeshwa kwa misingi ya ubaguzi. Wanachi wote bila kuzingatia rangi, dini au kabila walipata fursa ya kusomesha watoto wao katika shule waliyoipenda.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Elimu ileile iliyokataliwa imejirudia japokuwa si kwa namna ileile. Katika ngazi ya eleimu ya msingi kuna matabaka mawili yaani shule za "English medium" na zile za kawaida. Katika ngazi ya sekondari matabaka makubwa ni mawili; shule za serikali na za binafsi. Shule serikali nazo zimegawanyika makundi mawili zile za kata na za zamani. Shule za private zinaweza kuwa katika matabaka kulingana na ada inayotelewa.[/FONT] [FONT=&amp]
  Matabaka katika elimu ni wazi kabisa. Shule nyingi ni duni na wanaosoma katika shule hizo wanatoka katika tabaka la chini. Baadhi ya shule ni za kiwango cha kati na wanaosoma huko ni watoto wanaotoka katika tabaka la kati. Shule chache zinatoza ada kubwa kama Feza, ST Marian n.k na watoto wanaosoma shule hizi wengi ni wa tabaka la juu.
  [/FONT] [FONT=&amp]
  Historia inatukumbusha kuwa wamisionari ndio walihusika sana na uanzishaji wa shule. Matokeo yake wakristo wengi walipata fursa ya kupata elimu tangu awali. Baada ya uhuru wengi wao wakawa katika nafasi nyingi katika sekta ya utumishi, uchumi na utawala. Hali hii ilizua malalamiko kutoka jumuiya ya waislamu hata sasa bado kuna malalamiko kuwa wanaonewa.[/FONT] [FONT=&amp]Mtu anayefikiri sawasawa atagundua kuwa elimu ni chombo muhimu sana katika ujenzi, usalama, na amani kwa taifa. Hii ina maana kuwa ni lazima itolewe kwa misingi ya usawa ili kila mtu aipate kwa kiwango kilekile anachopata mwenzake. Mtu ashindwe mwenyewe lakini si kwa kunyimwa fursa. Shule ziendele kuwepo lakini huduma iwe ni sawa na hii ni kazi ya serikali kwa pamoja na wazazi au wanachi.

  [/FONT] [FONT=&amp]Hali ya elimu ya sasa imeparaganyika. Matabaka yako wazi. Siku za baadae itakuwa kazi kweli kwani wanyonge wengi watakapogundua kuwa hawako katika siasa; hawamiliki uchumi n.k. na sababu zinatokakana na kubaguliwa wakati fulani katika elimu ‘watareact'; malalamiko yatakuwa mengi; wizi na ujambazi vitaongezeka pia fujo zitakuwa nyingi dhidi ya wale wanaopata elimu bora sasa. Nchi haitatulia.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Nisiishie tu kusema hayo, nitoe ushauri kuwa hatua za haraka zichukuliwe kuboresha elimu hasa katika shule za watu walio wengi. Pia mipango ifanywe kuponya majeraha kwa wale walioathirika na mfumo huu yaani wale waliomaliza katika shule hizo na hawakufaulu kabisa. Kwa kupitia taasisi kama ile ya Elimu ya watu wazima na Veta wanaweza kuandaliwa program fulani wakasoma na hatimae wakaweza hata kufika vyuo vikuu.

  Ninalosema si utani, kuna vijana wameichukia serikali, wazazi na hata wao wenyewe kwani kwa kupitia mfumo wa elimu uliopo wameshindwa kutimiza ndoto zao si kwa sababu hawana uwezo wa akili bali hawakupata fursa kama kuwa na walimu, vifaa, fedha n.k. kama ilivyo kwa wengine.[/FONT] [FONT=&amp]

  Serikali na wadau wote wahakikishe kuwa elimu inatolewa kikamilifu kama dozi ya malaria. Hebu fikiri kidogo: kama dakatri atapokea wagonjwa watatu wa malaria mmoja akampa dozi nzima ya vidonge ishirini na nne vya dawa mseto; mwingine vidonge 12 na.yule wa tatu kidonge kimoja unaona hapa ni mgonjwa mmoja tu ndiye atakayepona. Hali ya elimu Tanzania ni kama hiyo ni wachache sana wanapata elimu kikamilifu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Nimekaa katika sekta ya elimu muda mrefu na nimeona hatari iliyopo ndo nikaona nitoe dukuduku langu basi wenzangu ikiwa hoja yangu ina ukweli basi pimeni mapungufu nachieni maana binadamu hajakamilika bwana![/FONT]
   
Loading...