Elimu ya Tanzania katika karne ya 21

Elimu ya Tanzania katika karne ya 21

Nervousity

Member
Joined
Nov 3, 2017
Posts
21
Reaction score
14
Kumekuwepo na 'slogan' nyingi zinazotumika katika kutanabaisha umuhimu wa Elimu kama vile: Elimu ni ukombozi! Elimu ni kazi! Elimu kwa maendeleo! Elimu ni juhudi na maarifa n.k. Hii yote inalenga kuonyesha ni kwa kiasi gani elimu ni muhimu katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu.

Miaka ya mwanzo ya uhuru wa Tanganyika yaani 1961, ujinga uliorodheshwa na waasisi wa taifa letu kama miongoni wa maadui wa maendeleo. Kwamba ikiwa jamii ingeondokana na ujinga basi jamii ya Watanganyika na Tanganyika kwa ujumla ingekuwa imepiga hatua mojawapo ya maendeleo. Kwa kutambua hilo serikali ilitumia njia kadhaa wa kadhaa kuhakikisha kuwa kila aliyestahili kupata elimu ya msingi anaipata na hivyo kuja na mpango wa Elimu kwa Wote (Universal Primary Education). Yaani kila mtoto aliyekuwa amefikia umri wa kuanza shule yaani kuanzia miaka 7 na kuendelea alitakiwa kuanza shule. Wakati huo ilishuhudiwa wanafunzi ambao wengine walikuwa na umri mkubwa hata wa kuwa sekondari lakini walidahiliwa kuanza darasa la kwanza. Wakati huo ilikuwa kila mwanafunzi ajue Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Kana kwamba haitoshi ulianzishwa mpango wa elimu ya watu wazima ili kutoa fursa kwa watanzania wa umri mkubwa kupata fursa ya kujifunza kusoma na kuandika. Ikashuhudiwa madarasa ya watu wazima yakianza mengine chini ya miti, kwenye nyumba za ibada, ofisi za serikali n.k. Hii yote ililenga kutoa fursa kwa kila Mtanzania kupata Elimu ya Msingi ambayo si tu ingemletea maendeleo yeye mwenyewe na nchi bali ingemsaidia kupambana na maradhi na umasikini. Katika miaka hiyo yote elimu ya sekondari haikuwa kipaumbele sana.

Elimu ya karne hii ya 21 globally ni ya sayansi na teknolojia. Je, mpango kazi wa nchi yetu katika sekta ya Elimu kwa karne hii ni upi? Je, bado tunaamini katika KKK pekee kwa elimu ya msingi? Au KKK za kisayansi na kiteknolojia? Je, Ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa sekondari tu? Au kuwa na wahitimu wa vyuo vikuu wasiokuwa na ajira rasmi? Ni elimu bure kwa wote bila kuwa na mipango? Kuwa na wahitimu wengi wa kidato cha nne ambao hawaendelei na elimu ya kidato cha tano na sita wala chuo kikuuu?

Watoto wetu wapendwa waliohitimu kidato cha sita na wengine Astashahada na Stashahada na kupata udahili katika vyuo vikuu vyetu wamekosa mikopo. Je, hawa wachache waliopata mikopo tunataka wakishahitimu wazibe pengo lipi (Upungufu)? Au kwa kuwa ndio idadi pekee mbayo serikali imeweza kumudu kugharamia masomo yao? Hawa waliokosa mikopo wataandaliwa utaratibu mwingine wa kusoma au ndio basi? Kwani kwa sasa ELIMU YETU YA MSINGI INAKUSUDIA NINI? SEKONDARI JE? na VYUO VIKUU VIPI?

Nadhani tutakuwa tunakosea ikiwa tunajenga mashule mengi ya sekondari, tuna wanawahitimu wengi wa kidato cha sita na vyuo vikuu ambao ama wamekosa mikopo ama wamekosa ajira; yaani kama taifa hatuna mipango. Tutaendelea kuhimiza watoto wetu wafaulu waende sekondari halafu wakifaulu hakuna mikopo? So what?

Hivi ni sahihi katika karne hii serikali kuendelea kuhimiza kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi? Yaani serikali ingependa kuona idadi ya ufaulu inaongezeka mwaka hata mwaka halafu mwisho wa siku wanafunzi hawa wanakosa mikopo kwa kuwa siyo yatima, wazazi wao siyo maskini? What actually do we want to achieve in education at present?

Katika karne ya 21 tunazungumzia kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba? Hivi elimu yetu ya sasa inalenga kufaulisha wanafunzi na si kuwapatia ujuzi? Ujuzi unapimwa kwa ufaulu? Kwani ufaulu unaongeza tija kwenye uzalishaji? We need to change our mind set!

Elimu ya Tanzania karne hii ya 21 inalenga nini?
 
Ili Tanzania iendelee inahitaji kuwa na maprofesa wangapi? Hawa wachache waliopo wana mchango gani?
 
Daaaah inasikitisha kwakweli yani tupo kama Kuku aliyekatwa kichwa. Bora liende tu.
 
Back
Top Bottom