ELIMU YA BURE

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,660
1,801
Kwanza, naamini hili ni jambo linalowezekana. Kuna nchi kadhaa zinatoa elimu ya bure tena zenye mazingira kama Tanzania. Wakati wa Mwalimu elimu ilikuwa bure.
Ila hili, kama mambo mengine ya taifa, halipaswi kufanywa kwa 'diktat' bila ya kuliwekea misingi. Ni dhahiri kuwa kwa taarifa za karibuni, JP litamshinda hili na itafikia wakati atalazimika kumeza 'humble pie'. Kwa nini? kwa sababu amelifanya ni jambo la kisiasa zaidi kuliko kuwa jambo la kimkakati na sera.
Ilikuwa vizuri alianze kwa taratibu. Kwa mfano, kuzidisha ruzuku ya serikali 'subsidies' itayopelekea kupunguza karo kwa wanafunzi.
Siku zote hushangaa, kwa nini viongozi wa Tanzania yaelekea wamenyimwa akili na hekima. Tanzania ni nchi yenye vipato tofauti sana kwa wananchi wake kutokana na maeneo wanayoishi. Hasa hasa kuna tofauti kubwa kwa wanaoishi vijijini na wale waishio mijini. Kwa nini kusiwe na sera za serikali zinazolitambua hilo? Leo mtu wa Dar ambaye kipato chake ni kikubwa hununua sukari kama anavyonunua mtu wa Biharamulo.
Kama ningekuwa kiongozi wa Tanzania, ningelikabili suala hili la elimu bure kama ifuatavyo;
Shule zilizo Dar, Mwanza, Arusha, Shinyanga, Mbeya: wanafunzi watalipa ada ya shs. laki moja kwa mwaka kuanzia darasa la tano Primary. Hizi zitalipwa kwa mikupuo mine, across the board. Marufuku michango, na hakuna fees kuanzia darasa la kwanza - 4
Sekondari watalipa laki 2 kwa mwaka across the board, yaani hadi form 6.
Makao makuu ya mikoa: Elfu 50 kwa mwaka Primary, laki moja Sekondari.
Makao makuu Wilaya: Elfu 30 Primary, elfu 50 Secondari
Chini ya hapo (vijiji, tarafa etc): elfu 10 au bure ....
Obviously, serikali ingejaliza (subsidise), lakini ingekuwa na maduhuli pia.
Ningeweka 'msamaha' kwa wale wote watakaothibitika kuwa kipato chao hakiwezi kabisa kumudu hata ada hiyo- hii ni kudhamini kila mtoto anakuwa shule.
Ningeendelea na mfumo huu kwa miaka mitano huku nikizatiti infrastructure, shule, libraries, n.k.Baada ya miaka hiyo naanza kupunguza kwa nusu. Wale waliokuwa wakilipa laki itashuka hadi 50,00 na hivyo hivyo. Katika kipindi cha miaka 20 nita phase out school fees completely na hiyo ingewezekana bila matatizo.
Kukurupuka tu na kutoa 'diktat' elimu bure, kutafeli na baadaye ije isemekane elimu bure haiwezekani, ilhali ni ukosefu wa fikra pana na mipango ndio uliofelisha.
 
Back
Top Bottom