Je, ushawahi kujiuliza tofauti kati ya AIRPLANE or AEROPLANE?
Au AIRCRAFT na FLIGHT?
Ingawa maneno haya yote kwa Lugha ya kiswahili yanaweza kumaanisha Ndege, lakini hizi ndiyo tofauti zake;
Airplane:
β
Neno hili hutumika sana katika Kiingereza cha Marekani, likimaanisha chombo cha usafiri wa anga chenye mabawa tulivu (Fixed wing)
Aeroplane:
β
Neno hili hutumika katika Kiingereza cha Uingereza na lina maana sawa na 'Airplane' tofauti ni matamshi kati ya Nchi na Nchi.
Aircraft:
β
Hili ni Neno pana zaidi likimaanisha ndege zote au mashine yoyote yenye uwezo wa kuruka angani.
Inajumuisha Ndege za kawaida, Helikopta, Glider, Drones, Puto, Tiara n.k.
Flight:
β
Neno hili linamaanisha safari au kitendo cha ndege kuruka.
Linaweza kumaanisha safari ya anga iliyoratibiwa mfano 'Flight EK 200' au tukio halisi la kuruka kwa ndege yeyote.