Kwa uzoefu wangu mpaka sasa, nimegundua tatizo la elimu yetu halipo kwenye mitaala bali lipo kwenye utekelezaji wa hiyo mitaala. Mfano wanafunzi hawasomi namna ya kufanya practicals ila wanajifunza kufoji ingawa mitaala imeeleza vizuri namna wanavyotakiwa kujifunza hizo practicals. Sasa baadae mwanafunzi akishindwa wanaanza kusingizia mitaala. Hasa shule zetu za kata ndio zinaongoza kwa kutofuata mitaala, Wanafunzi wanajisomea hovyo hovyo tu.
Elimu ya A level ni kwa ajili ya maandalizi ya kwenda hatua nyingine mbele na sio kuishia hapo, nchi ambazo hazina A level basi lazima mwaka wa kwanza chuo utumike kuwafundisha wanafunzi kozi ambazo walizikosa kwa kutosoma A level. General studies ya A level iko vyema katika kupanua uelewa wa mambo mengi lakini wanafunzi wanaichukulia poa, sasa hapo tatizo la mitaala lipo wapi?.