Kiwalani finest
Senior Member
- Jul 6, 2024
- 116
- 85
ELIMU CHACHE TULIZO NAZO
TUZITUMIE KUWANUFAISHA WENGINE.
Wanaccm wenzangu Elimu ya kujua Mambo mbali mbali ni ya Muhimu katika maisha YETU ya kila siku pia na maisha yetu ya baadae TUTAKAPOIAGA DUNIA HII INAYOMEZA WENGI WAKAPUMBAA NA KUMSAHAU MOLA WAO.
Tukisoma Katiba ya CCM 1977 toleo la 2017 uk 143 kifungu cha 06 kinasema,
Nitajielimisha kwa kadri ya Uwezo wangu na KUITUMIA ELIMU yangu kwa faida ya Wote.
Wanaccm wenzangu hii ni AHADI TULIYOAHIDI ni lazima kila Mmoja wetu ATIMIZE AHADI ili tuonyeshe utii kwa Mambo ya msingi tunayokubaliana kuyafuata vinginevyo tutaonekana WANAFIKI.
Nakumbuka Oct 2020 Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa Bunju aliwahi kusema ninamnukuu,
" Ahadi zangu Mimi si za Uongo, AHADI ZANGU SI ZA UONGO, Msema Kweli ni Mpenzi wa Mungu"
Wanaccm wenzangu kwa kauli hiyo ya M/kiti wetu inatupa wajibu na SISI kutekeleza ahadi zetu na kuwa wakweli ili tuishi TUKIPENDWA NA MUNGU WETU.
Wanaccm wenzangu tukisoma pia katiba ya CCM 1977 Toleo la 2017 uk 09 ibara ya 15(6)
inasema,
" Kila Mwanachama atakuwa na WAJIBU wa KUJIELIMISHA KWA KADRI YA UWEZO WAKE na KUITUMIA ELIMU HIYO KWA faida ya wote."
Wanaccm wenzangu CHANGAMOTO NYINGI KATIKA BARA LA AFRIKA , NYINGI HUTOKANA NA UKOSEFI WA ELIMU YA KUTOSHA MIONGONI MWA WAAFRIKA.
NI WAJIBU WETU KUJITOA KWA AJIRI YA WENGINE ILI TUWAELIMISHE.
Niliwahi kusoma Kitabu cha Binadamu na Maendeleo uk 66
Mwl JK Nyerere aliwahi kuandika,
"Sisi watu wa Afrika si watu wenye Elimu kubwa na wala SIAMINI kwamba watu walio wengi katika nchi yeyote WAMEELIMIKA vya kutosha karika Mambo ya Siasa."
Ni lazima sasa Wanaccm Kwa UMOJA WETU TUAMUE KUUPIGA VITA UJINGA KWA KUTOA ELIMU KWA WENZETU BILA KUJALI ITIKADI YA MTU.
Nakumbuka oct 2019 Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa Songwe aliwahi kusema ninamnukuu,
" Baba wa Taifa alizungumza juu ya MAADUI WATATU, na aliwataja hayati Baba wa Taifa letu , Maadui hao watatu bado HAWAJABADILIKA."
" Ambao ni UJINGA, Maradhi, na Umaskini. Hawa ndiyo Maadui Watatu wakubwa katika nchi yetu lakini pia katika nchi zingine."
" Suala la UJINGA ambalo linaendana na kutoa Elimu tumeanza kulishughulikia kwa nguvu zote."
Mwisho wa kunukuu.
Wanaccm wenzangu TUNALO TATIZO KUBWA
MTU ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA KUTOA ELIMU MARA NYINGI HUCHUKIWA NA KILA MTU.
HUU NI UJINGA MKUBWA AMBAO NI LAZIMA TUDHAMIRIE KUUACHA.
MTOA ELIMU ANAKUWA NA MAADUI WENGI HUKU AKIPANGIWA MIZENGWE YA KUTOSHA.
KUENDEKEZA TABIA HIZI NI UJINGA .
Nakumbuka Mwaka 2018 Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa MIKUMI aliwahi kusema ninamnukuu,
" Ukitaka KUWATAWALA WATU wanyime Elimu."
Mwisho wa kunukuu.
Wanaccm wenzangu NA TUANZE SASA KILA MMOJA WETU ANACHOKIJUA NA AWE TAYARI KUMFUNZA MWINGINE PASIPO KUWAHOFIA WACHACHE AMBAO KAZI YAO NI KUWAKATISHA TAMAA WENZAO KWA MASLAHI YAO YENYE VIASHIRIA VYA
UBEPARI.
Tukisoma MAANDIKO MATAKATIFU ya Mwenyezi Mungu katika Kitabu cha Muntakhab Ahadith (Green Cover) uk 313 kifungu cha 45
Maandiko yanasema,
" Abu hurairah Radhiallahu Anhu amesimulia kuwa Rasulullahi Swallallahu Alaihi Wasallam amesema,
" Mfano wa mtu ambaye anatafuta Elimu ya Dini na kisha HAIFIKISHI kwa WENGINE ni Mfano wa yule ambaye AMEKUSANYA HAZINA lakini HAITUMII na kunufaika kutokana nayo."
Tukisoma tena Kitabu hiki cha Maandiko Matakatifu uk 302
Mwenyezi Mungu anatuambia,
" Safwari bin Assal Al-Muradi Radhiallahu Anhu amesimulia kuwa ,
' Nilikwenda kwa Nabii Swallallahu Alaihi Wasallam, naye alikuwa Msikitini, akiwa amejinyoosha kwa shuka lake lenye mistari ya rangi nyekundu.
Nikasema,
" Ewe Rasulullahi nimekuja kutafuta Elimu.
Akasema,
"Karibu Ewe mwenye kutafuta Elimu kwa hakika Malaika humfunika mwenye kutafuta Elimu kwa mbawa zao na kisha hukusanyika mmoja juu ya mwengine mpaka wanafika mbinguni, kwa ajili ya Mapenzi ya Elimu inayotafutwa."
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mathias Mugerwa Kahinga
🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿