Elimu nchini Tanzania

Rgrs Nd

Member
Jul 18, 2022
14
2
UTAANGULIZI

Kwanza kabisa tunapaswa kuelewa tunaposema elimu tunamaanisha Nini?Inaweza kuwa tofauti na unavyofikiri Lakini maana halisi ya elimu tunasema ni taarifa zilizo rasmi ambazo Huwa zimebeba maudhui yenye kulenga kuboresha zaidi au kupunguza kama sio kuondoa kabisa madhara yanayosababishwa na kanuni au tabia Fulani tulizojijengea wenyewe.

Lengo kubwa kabisa la elimu tunazoona zikitolewa Katika maeneo mbalimbali Huwa na lengo la kuleta mabadiliko miongoni mwa wanajamii.Sasa hapa ninachotaka kuzungumzia ni juu ya mfumo mzima wa elimu unaotolewa mashuleni na vyuoni,Katika kuzungumzia Kuna mambo mawili nitakayogusia nayo ni;Changamoto zilizopo na Kwa jinsi gani zimepelekea wahusika(wanafunzi)kushindwa kunufaika nayo,pia Nitatoa mapendekezo ambayo Kwa imani na uelewa wangu naona yanaweza kuwa na mchango Kwa jamii.


CHANGAMOTO ZILIZOPO

1. Ukosefu wa wataalamu wenye kuweza kuthibiti ubora

Kukosekana Kwa wathibiti ubora Hawa kumepelekea kuwepo na idadi kubwa ya walimu wasiofahamu juu ya Namna Bora ya ufundishaji,pia kumekuwa na ongezeko na vitendo ovu ambavyo vimeathiri na hata kuuwa ndoto za watoto mashuleni kama vile ubakaji n.k yote hii ni sababu ya uwepo wa walezi mashuleni wasiokuwa na ubora stahiki yaani wamekosa maadili ya kazi.

2. Mabadiliko ya mtaala

Serikali imeweka juhudi nyingi Katika ufanyaji wa mabadiliko ya mtaala lengo likiwa ni kuboresha mfumo mzima wa elimu nchini.Changamoto iliyopo ni ukosefu wa ufuatiliaji wa ni Kwa kiasi Gani mitaala hii imechangia Katika kuleta maendeleo badala yake viongozi wamekalia kubadikisha pasipo kuzingatia maoni ya wahusika au wale wanaolengwa kunufaika

3. Idadi ndogo sana ya vyuo vinavyojihusisha na utoaji wa kozi za afya.

Nikiwa kama mhanga,ukifuatilia mwongozo wa TCU juu ya alama za mwisho ambazo zitamwezesha mhusika kujiunga na vyuo vilivyopo nchini Kwa kozi za afya utaona alama ya mwisho ni "D" tatu Katika masomo ya sayansi yaani Physics,Chemistry,Biology.Sasa uwepo wa idadi ndogo ya vyuo vya serikali kumepelekea baadhi yetu kukosa nafasi halafu wakati huo utaisikia serikali ikisema tunahitaji watu makini sana yaani wale wenye ufaulu daraja la kwanza walipohitimu kidato Cha sita.

4. Ukosefu wa mikopo ya elimu ya juu

Changamoto hii imepelekea baadhi ya watu kuacha kabisa masomo kutokana na Hali duni za Maisha kwani ni gharama kubwa sana inahitajika wakati huo unakuta baadhi Yao walikuwa na mategemeo makubwa kupitia elimu hii ya juu. Wengine imewawia vigumu kinapofika kipindi Cha kufanya tafiti(research)kwani hujikuta wanakosa lile fungu ambalo baadhi hulipata hivyo kushindwa kufanya kazi hiyo Kwa weledi.

5. changamoto ya kuzuiwa kufanya mitihani ya kumaliza muhula vyuoni pindi unaposhindwa kukamilisha malipo ya ada

Hii imekuwa ni changamoto kubwa sana japo serikali imekwisha kutoa tamko kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kufanya hivyo,vitendo hivi vinaonekana Katika baadhi ya vyuo tu hii inaonyesha tu kuwa vyuo hivyo ni kama vimelenga kujitafutia mapato tu kupitia ada na wakati huo huo ni vya serikali


Mapendekezo yangu;

Kwanza kabisa kama kijana mta zania ninapendekeza kuwa,serikali unapaswa kuhakikisha Kuna wathibiti ubora ambao watahakikisha wale wote ambao watapewa au kuaminiwa kufanya kazi Katika sekta hii ya elimu wanakuwa na vigezo stahiki Ili kuepusha baadhi ya mambo hatarishi.

Pia serikali inapswa kuwa na mfumo utakaoiwezesha kupima mafanikio Mara baada ya ufanyaji wa mabadiliko Katika mitaala na kuwa tayari kupokea mapendekezo kutoka Kwa wahusika yaani wanafunzi.

Pia Serikali inapswa kuangalia juu ya suala la idadi ya vyuo hivi vya afya Ili kuwezesha upatikanaji wa wataalamu juu ya masuala ya afya ambao hata watakapokosa ajira basi jamii inaweza kuwatumia Kwa namna nyingine yoyote ile kimaendeleo zaidi.

HITIMISHO

Ni Matumaini yangu kupitia uandishi huu Kuna kitu Cha ziada ambacho kama serikali na hata wahusika Katika nafasi Fulani Fulani za serikali wataweza kujenga fikra na mtazamo mpya juu ya maendeleo ya taifa Kwa ujumla.


Niko tayari Kwa mjadala utakaoinuka juu ya uandishi huu.....
 
Back
Top Bottom