Elimu hasa kwenye shule zetu za umma iko taabani, viwango vya elimu vinashuka, shule zetu zimegeuka kuwa viwanda vya kuzalisha ujinga. Uwezo wa wahitimu kuchambua mambo na kujenga hoja sio wa kuridhisha, na suala zima la ubunifu na uwajibikaji limekuwa hafifu. Kuna ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika achilia mbali uwezo wa kuongea lugha za kimataifa ambazo zinatumika kufundishia. Ubunifu wenye tija kwenye nyanja karibia zote umekuwa adimu hivyo kuzidi kuchangia ongezeko la umaskini kwenye taifa letu.
Nini chanzo chake?
Nini kifanyike? (hapa tuchambue kwa mapana)
Naomba kuwasilisha.