Timeshajadiliana sana hapa jukwaani kuhusu hivi viumbe, asili yake tabia mienendo na utendaji wake.
. Hivi ni viumbe roho kwa maana ya kwamba havina umbo kamili la kimwili
. Huwinda miiili ya kufanya makazi yake sehemu za majini, makaburini milimani na hata kwenye misitu minene
. Kuna mkanganyiko kuhusu lifespan yake... Kuna dhana kuwa mapepo hufa lakini dhana nyingine ikipinga kwa muktadha wa kwamba hawa ni viumbe roho na roho haifi...
.Pepo bila kupata makazi ya kuishi hutaabika na kuwayawaya huku na kule mpaka yapate sehemu ya kutua
Hebu tuone pepo/mapepo kwa muktadha wa manabii na mitume.. Mapepo yatolewayo kwa waumini kwenye ibada zao
Case study ya Rose Mhando
Pepo ni viumbe roho wenye nguvu sana na anapoingia mahali na kufanya makazi basi kumtoa, kuwatoa si kazi rahisi.. Na unapomfukuza hapo alipo humwambii tu TOKAA bali inabidi umwambie aende wapi
Pepo anapoingia mahali huingia pekeyake lakini kadiri nuda unavyosonga huwaalika na pepo wengine kuja kuishi pamoja
Mazingira haya ya kuishi pamoja kuna wakati husababisha kuleta vita ya umiliki kwenye mwili husika..... Hapa mhanga mwenye mwili atapata tabu kwa vita isiyomhusu
Vilevile kuna wakati hawa waombeaji hufanya michezo ya kuwaalika mapepo kwa mkono mmoja na kuwafukuza kwa mkono mwingine... Hii humjenga na kuonekana ana karama kubwa....
Kwenye imani ya Kikristo tunaona Bwana Yesu akiwatimua mapepo.... Kwa kutumia mfano wake huu unaweza kupata maarifa mapya... Je alifanyaje?
Tunaambiwa akiwa NG'AMBO ya bahari alikutana na mtu aliyetoka MAKABURINI mwenye PEPO MCHAFU na makao yake yalikuwa MAKABURINI
Mtu huyu hakuna hata mmoja aliyeweza kumfunga tena hata kwa minyororo kwakuwa alishafungwa maranyingi kwa pingu na minyororo lakini akaikata minyororo na kuvunja pingu
Nuda mwingi alikuwa MAKABURINI na MILIMANI akipiga kelele na kujikatakata na mawe
Basi akamwona Yesu AKAMSUJUDIA kisha akasema NAKUAPISHA USINITESE..... Lakini Yesu akamwamuru PEPO amtoke mtu yule.... PEPO yule aliyejitambulisha kama LEGIONI (tafsiri ya wingi) akamsihi Yesu asiwapeleke nje ya mipaka ya nchi ile (kumbe hata wao wana mipaka)
Basi wakamsihi awapeleke kwenye kundi la NGURUWE, wapate kuwaingia wao.... YESU AKAWAPA RUHUSA... Nao wkawaingia NGURUWE wale na kutimkia bondeni majini.... Jumla ya mapepo/NGURUWE yalikuwa 2000
Hiyo ndio shughuli pevu ya mapepo... Pepo linalomtoka mtu ndani ya dakika 2 hilo ni feki ama la kualikwa... Lakini hata kama leo hii kuna mapepo basi ni malaini na nyoronyoro mno.... Mapepo yanayoruhusu mtu aoge na kuvaa vizuri, mapepo yanayoruhusu mtu ajitambue na kusimulia kila kitu... Haya ni mapepo ya kileo, kidigitali na kinyangema kweli....
Nimemaliza......
Hakika siwezi kufahamu kila kitu na nikisema nafahamu vyote itabidi nipelekwe kupimwa bulangataMarko 16:17 na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini, kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.
Ndugu yangu Mshana Jr kuna vitu umegusia ila vingine huvifahamu.
Ysu alitoa pepo kwa watu wengi sana ukisoma zile injili utaona sema nimekosa mistari ningekuwekea hapa.
Pepo wapo na wanatoka kwa uweza wa Yesu Kristo Mwana wa MUNGU.
Uwepo wa manabii feki ni kweli hili limewekwa wazi kwenye injili pia kwa hiyo mkuu upo sahihi kabisa.
Naconnect dot na uzi wako huu Elimu juu ya pepo/mapepo - JamiiForums
Ni kweli mkuu dunia ina mengi sana... but ni vyema kusaidiana namna hii.Hakika siwezi kufahamu kila kitu na nikisema nafahamu vyote itabidi nipelekwe kupimwa bulangata
Hayo atakua kapewa na nabii feki mwenyewe kamrushia then kayatoa, usicheze na roho waovu ndugu.Kwa tafsiri ile ya Bible ni ngumu kuweza kutofautisha kwakuwa kwa asilimia 90 viashiria vinafanana
Lakini kwa tafsiri ya kileo tofauti ziko wazi kabisa
Kichaa utamkuta mitaani mchafu kabeba mizigo isiyoeleweka, anaongea pekeyake nknk
Mwenye mapepo utamkuta kaondoka nyumbani safi kabisa na akili zake, kaoga kapendeza akifika kwa nabii akianza kuombewa mapepo yanalipuka lakini baada ya misa anakuwq fresh kabisa mpaka siku nyingine
Ni biblia gani hiyo yenye marko 16:17Marko 16:17 na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini, kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya.
Ndugu yangu Mshana Jr kuna vitu umegusia ila vingine huvifahamu.
Ysu alitoa pepo kwa watu wengi sana ukisoma zile injili utaona sema nimekosa mistari ningekuwekea hapa.
Pepo wapo na wanatoka kwa uweza wa Yesu Kristo Mwana wa MUNGU.
Uwepo wa manabii feki ni kweli hili limewekwa wazi kwenye injili pia kwa hiyo mkuu upo sahihi kabisa.
Naconnect dot na uzi wako huu Elimu juu ya pepo/mapepo - JamiiForums
Mzee mmoja alishafariki kwa sasa, Munga Tehenani alikuwa akiandika sana juu ya mada hizi. Na kwa kweli alikuwa vizuri. Mshana ana vitu ila........Hahaha mkuu tukianza kuwalaumu wazungu kwa kutokufahamu kwetu, nikuwaonea. Nimesema hivyo kwa sababu. Kule wana tibu bipolar patients, hysterical patients, mental disabled patients, na hata depression na stress wanatibu. Huku vyote hivyo tuna sema huyo kichaa,kaheuka, karogwa, katupiwa jini, ana mapepo n.k. yani mapungufu yetu ya ufahamu tuna tafuta wa kumlaumu. Tatizo letu kubwa bado ni elimu ya ufahamu wa haya mambo, na hasa upungufu wa wataalamu, kama psychiatrist na clinical psychologist. Mtu anaanza kucheka hovyo, anapelekwa kuombewa eti anapepo, hiyo ndio early prognosis yetu, hatutaki kujifunza the science/physiology behind it. Tuna fanya simple conclusion kwa vitu vinahitaji scientific explanations, vingi vina hitaji proper diagnosis kujua what and why, lakini hatuna hizo diagnostic tools tuna simplyfy eti mapepo hayo, kichaa huyo. It shouldn't be like that mkuu. Sasa hapo ndio tunazalisha hawa manabii feki, wanatuibia tunawalaumu. Hatutaki ku invest kwenye R&D sisi tunataka wengine wafanye sisi tutumie. Ok hata reserch zilizofanywa na kuwa proved hatuzisomi tukazitumia, tukishindwa kutibu ama kwa kutokujua/kufahamu, au kushindwa kudiagnose tunasema, huu ugonjwa wa kienyeji, ohoo mapepo. Ningefurahi kama nasisi tungeshughulisha vichwa vyetu kwenye hayo mambo, tatizo yunayaona eti ni madogo, tunajidai sisi huwa tuna deal na mambo makubwa tu. Kumbe hata hayo makubwa bado hatuwezi. Mkuu ukiacha mbali taaluma yako ya MA yuo can be be a self made clinical psychologist. Tuendelee na mada.
Siyo mbaya ukishare nasi hizo mada, lengo humu ni kulimika sio kushindana.Mzee mmoja alishafariki kwa sasa, Munga Tehenani alikuwa akiandika sana juu ya mada hizi. Na kwa kweli alikuwa vizuri. Mshana ana vitu ila........
Timeshajadiliana sana hapa jukwaani kuhusu hivi viumbe, asili yake tabia mienendo na utendaji wake.
. Hivi ni viumbe roho kwa maana ya kwamba havina umbo kamili la kimwili
. Huwinda miiili ya kufanya makazi yake sehemu za majini, makaburini milimani na hata kwenye misitu minene
. Kuna mkanganyiko kuhusu lifespan yake... Kuna dhana kuwa mapepo hufa lakini dhana nyingine ikipinga kwa muktadha wa kwamba hawa ni viumbe roho na roho haifi...
.Pepo bila kupata makazi ya kuishi hutaabika na kuwayawaya huku na kule mpaka yapate sehemu ya kutua
Hebu tuone pepo/mapepo kwa muktadha wa manabii na mitume.. Mapepo yatolewayo kwa waumini kwenye ibada zao
Case study ya Rose Mhando
Pepo ni viumbe roho wenye nguvu sana na anapoingia mahali na kufanya makazi basi kumtoa, kuwatoa si kazi rahisi.. Na unapomfukuza hapo alipo humwambii tu TOKAA bali inabidi umwambie aende wapi
Pepo anapoingia mahali huingia pekeyake lakini kadiri nuda unavyosonga huwaalika na pepo wengine kuja kuishi pamoja
Mazingira haya ya kuishi pamoja kuna wakati husababisha kuleta vita ya umiliki kwenye mwili husika..... Hapa mhanga mwenye mwili atapata tabu kwa vita isiyomhusu
Vilevile kuna wakati hawa waombeaji hufanya michezo ya kuwaalika mapepo kwa mkono mmoja na kuwafukuza kwa mkono mwingine... Hii humjenga na kuonekana ana karama kubwa....
Kwenye imani ya Kikristo tunaona Bwana Yesu akiwatimua mapepo.... Kwa kutumia mfano wake huu unaweza kupata maarifa mapya... Je alifanyaje?
Tunaambiwa akiwa NG'AMBO ya bahari alikutana na mtu aliyetoka MAKABURINI mwenye PEPO MCHAFU na makao yake yalikuwa MAKABURINI
Mtu huyu hakuna hata mmoja aliyeweza kumfunga tena hata kwa minyororo kwakuwa alishafungwa maranyingi kwa pingu na minyororo lakini akaikata minyororo na kuvunja pingu
Nuda mwingi alikuwa MAKABURINI na MILIMANI akipiga kelele na kujikatakata na mawe
Basi akamwona Yesu AKAMSUJUDIA kisha akasema NAKUAPISHA USINITESE..... Lakini Yesu akamwamuru PEPO amtoke mtu yule.... PEPO yule aliyejitambulisha kama LEGIONI (tafsiri ya wingi) akamsihi Yesu asiwapeleke nje ya mipaka ya nchi ile (kumbe hata wao wana mipaka)
Basi wakamsihi awapeleke kwenye kundi la NGURUWE, wapate kuwaingia wao.... YESU AKAWAPA RUHUSA... Nao wkawaingia NGURUWE wale na kutimkia bondeni majini.... Jumla ya mapepo/NGURUWE yalikuwa 2000
Hiyo ndio shughuli pevu ya mapepo... Pepo linalomtoka mtu ndani ya dakika 2 hilo ni feki ama la kualikwa... Lakini hata kama leo hii kuna mapepo basi ni malaini na nyoronyoro mno.... Mapepo yanayoruhusu mtu aoge na kuvaa vizuri, mapepo yanayoruhusu mtu ajitambue na kusimulia kila kitu... Haya ni mapepo ya kileo, kidigitali na kinyangema kweli....
Nimemaliza......
Malizia tu usijali.... Kumbuka Munga alikuwa anaandika kwenye gazeti mimi naandika mtandaoni kwenye mijadalaMzee mmoja alishafariki kwa sasa, Munga Tehenani alikuwa akiandika sana juu ya mada hizi. Na kwa kweli alikuwa vizuri. Mshana ana vitu ila........
Uko sahihi kabisa ila hata hivyo mapepo ya siku hizi dhaifu sanaMshana Jr pepo kumtoka mtu kwa wepesi inategemeana na Nguvu za Mungu alizonazo mtu husika, tunaona Mtume Paulo kivuli chake tu kilitumia kuwatoa pepo, nguo zake tu watu walipona, dhana ya pepo kutoka ndani ya dk 2 napingana nayo
Nadhani kuna tofauti kwakuwa kiasili majini nafikiri yameumbwa kwa moto
Uko sahihi kabisa ila hata hivyo mapepo ya siku hizi dhaifu sana
Hapo sasa, kwa mfano kuna rafiki yangu, alipata ajali ya gari, alijigonga kichwani.Hahaha mapepo HUWA SIYAAMINI. Unajua kuna watu wako Hysterical, wanacheka hovyo, au kulia hovyo au mara kwa mara, na hawaogopi kitu. Makanisani wanasema huyo mtu ana Mapepo. Hospitali wataalam wa vichaa wana sema huyo mtu ana hysteria. Sasa wewe unasemaje?!
Hahaha pepo la magari labda, nchi hii wakishindwa kudiagnose ugonjwa eti unakua umerogwa, au unamapepo.Hapo sasa, kwa mfano kuna rafiki yangu, alipata ajali ya gari, alijigonga kichwani.
Baada ya hapo alipoteza fahamu, hata baada ya kurudisha fahamu, amekua na tabia hizo wanazoziita mwezi mchanga, sasa huyu nae watasema ana pepo wa aina gani.