Elimu juu ya pepo/mapepo

Hewaaaa sasa umeanza kusogea kwenye mambo yako mkuu. Mimi nina swali Kunatofauti gani kati ya Mgonjwa wa akili(kichaa) na Mtu mwenye mapepo? Hapo juu uliongelea huyo aliyetolewa mapepo na yesu, kuna wahubiri wengine husema alikuwa Kichaa, wengine husema mapepo. Hapo huwa nakosa dermacation ya hizo tafsiri mbili, naomba msaada.
 
Niliuliza swali sijui limepotelea wapi mkuu, Kuna tofauti gani kati ya mgonjwa wa akili(Kichaa) na Mtu mwenye Mapepo, unawafahamu vipi na unawatufautishaje?!
 
[emoji144][emoji144][emoji144]
Niliuliza swali sijui limepotelea wapi mkuu, Kuna tofauti gani kati ya mgonjwa wa akili(Kichaa) na Mtu mwenye Mapepo, unawafahamu vipi na unawatufautishaje?!
Kwa tafsiri ile ya Bible ni ngumu kuweza kutofautisha kwakuwa kwa asilimia 90 viashiria vinafanana
Lakini kwa tafsiri ya kileo tofauti ziko wazi kabisa
Kichaa utamkuta mitaani mchafu kabeba mizigo isiyoeleweka, anaongea pekeyake nknk
Mwenye mapepo utamkuta kaondoka nyumbani safi kabisa na akili zake, kaoga kapendeza akifika kwa nabii akianza kuombewa mapepo yanalipuka lakini baada ya misa anakuwq fresh kabisa mpaka siku nyingine
 
Hivyo kutokana na maelezo yako, mapepo hulipuka anapoombewa tu?! Ni vipi yanamuathiri asipoombewa au kwenda huko kwa manabii?! Ukicha ndio Mental Disability? Mbona kuna wagonjwa wa ukichaa lakini wasafi au hawa hawa qualify kuitwa vichaa? Najua somo lako linahusu pepo.
 
Mapepo yapo ya aina nyingi kama ilivyo kwa vichaa
Kuna watu wanaishi na mapepo lakini hayalipuki mpaka zitokee situations fulani wasizopatana nazo....
Kuhusu ukichaa/uchizi kuna asilimia zikizidi ndio mtu huwekwa kwenye kundi la vichaa kamili, japo kuna machizi fresh na wale mwezi mchanga ambao hawa naona Kama vile wana connection na mapepo
 
Hahaha mapepo HUWA SIYAAMINI. Unajua kuna watu wako Hysterical, wanacheka hovyo, au kulia hovyo au mara kwa mara, na hawaogopi kitu. Makanisani wanasema huyo mtu ana Mapepo. Hospitali wataalam wa vichaa wana sema huyo mtu ana hysteria. Sasa wewe unasemaje?!
 
Kila mmoja yuko sahihi kwa kaliba yake
Hospital wanadili na mwili
Makanisani wanadili na roho.. Inawezekana kabisa wanamaanisha kitu kilekile ila kwa lugha tofauti... Kwakuwa pepo haliwezi kuonekana kwenye darubini za maabara na hysteria haiwezi kutosha kiroho
Mwisho wa siku mgonjwa ana tatizo
 
Unajua haya mambo yanazidi kukosa ukweli sayansi inapokomaa, Tunazidi kuona ukweli na uongo unaanza kujitenga. Umeenda nchi za watu, vichaa wa aina ya bongo, wengi wanatumia madawa na wanafunction normal. Bongo yetu hii vichaa wengi kwa sababu jamii haioni umuhimu wa kutibu magonjwa ya akili kama wanavyopigana na figo au moyo. Ndio maana utaona wanpata misaada mingi ya kutibu magonjwa hayo kutoka kwa donor country. Lakini siku tukianza kupata misaada mkuu hizi theories zote zita isha. Iwezekani, hysterical patient tuseme ana mapepo, na mental disabled tumuite kichaa.
Haya ya ulimwengu wa kiroho sijui, kutoa pepo ni usanii tu. Juzi wewe na mimi tulikubaliana kuhusu Rose Muhando, ule ni usanii tu. Kazidiwa na Unga, anazunguka Rehab, lakini bado anatafuta wakumlaumu, eti karogwa. Na wachungaji wake wanaamini sijui au ndio wanakamilisha usanii wao.
Naamini uwepo wa mungu/High power, siamini watu kuwa possed na mapepo. Labda kama niwe nachanganya mimi, Wengine huyaita mashetani, wengine huyaita maruhani.
Hizi huwa nahisi ni dilutional thoughts tu.
 
Uko sahihi kwa upande mmoja lakini kwa kutoa hukumu ya dilutional thought itakuwa hujatenda haki kwakuwa kuna mengi ambayo wazungu wanaya compress ili yaonekane mabaya kwa waafrika
 
mshana mambo yamegoma hayaendi kila naposhika kunafail si ajira si biashara nikampigia ustaadh mmoja akasema nina jini cheketu hii inakuwaje.....nimeogea sana chumvi baadhi ya mambo yanaenda ila haya ya kuhusu kipato cha maendeleo hakuna kunagoma....unaanzisha kitu kwa mtaji baadae from nowhere vitu vyote vinapururuka
 
Endelea na chumvi usiache
 
Uko sahihi kwa upande mmoja lakini kwa kutoa hukumu ya dilutional thought itakuwa hujatenda haki kwakuwa kuna mengi ambayo wazungu wanaya compress ili yaonekane mabaya kwa waafrika
Hahaha mkuu tukianza kuwalaumu wazungu kwa kutokufahamu kwetu, nikuwaonea. Nimesema hivyo kwa sababu. Kule wana tibu bipolar patients, hysterical patients, mental disabled patients, na hata depression na stress wanatibu. Huku vyote hivyo tuna sema huyo kichaa,kaheuka, karogwa, katupiwa jini, ana mapepo n.k. yani mapungufu yetu ya ufahamu tuna tafuta wa kumlaumu. Tatizo letu kubwa bado ni elimu ya ufahamu wa haya mambo, na hasa upungufu wa wataalamu, kama psychiatrist na clinical psychologist. Mtu anaanza kucheka hovyo, anapelekwa kuombewa eti anapepo, hiyo ndio early prognosis yetu, hatutaki kujifunza the science/physiology behind it. Tuna fanya simple conclusion kwa vitu vinahitaji scientific explanations, vingi vina hitaji proper diagnosis kujua what and why, lakini hatuna hizo diagnostic tools tuna simplyfy eti mapepo hayo, kichaa huyo. It shouldn't be like that mkuu. Sasa hapo ndio tunazalisha hawa manabii feki, wanatuibia tunawalaumu. Hatutaki ku invest kwenye R&D sisi tunataka wengine wafanye sisi tutumie. Ok hata reserch zilizofanywa na kuwa proved hatuzisomi tukazitumia, tukishindwa kutibu ama kwa kutokujua/kufahamu, au kushindwa kudiagnose tunasema, huu ugonjwa wa kienyeji, ohoo mapepo. Ningefurahi kama nasisi tungeshughulisha vichwa vyetu kwenye hayo mambo, tatizo yunayaona eti ni madogo, tunajidai sisi huwa tuna deal na mambo makubwa tu. Kumbe hata hayo makubwa bado hatuwezi. Mkuu ukiacha mbali taaluma yako ya MA yuo can be be a self made clinical psychologist. Tuendelee na mada.
 
Sasa unaposema case study ya Rose Mhando unamaanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…