Elimu isiyo rasmi

Elimu isiyo rasmi

Mwanambugulu

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2017
Posts
682
Reaction score
863
Wakuu habari zebu?
Niende moja kwa moja kwenye Mada
Nchi nyingi sana hasa ambazo hazina maendeleo Makubwa zimewekeza sana katika mfumo wa elimu ambao ni rasmi yani mtu anaenda shule anafundishwa lakini dhumuni kubwa ni kuja kuitumikia ile elimu katika nyanja mbalimbali hapa namaanisha kuajiliwa au raaah basi kujiajiri lakini si kwa kiasi kikubwa

Wanaofaulu Sana katika elimu hii ni wale watu wenye uwezo mzuri wa kukariri na kusoma bila Kuchoka pia wale wenyewe vipaji maalumu kabisa yani uwezo wa kuelewa masomo kwa haraka

Katika tafiti isiyo rasmi baadhi ya nchi zilizoendelea sana Kama America ,China,Japani,Korea na kwingine ingawa kuna elimu rasmi ila zimewekeza zaidi pia katika elimu isiyo rasmi

Hapa naongelea mambo Kama elimu ya fedha, umekezaji na mitizamo ya fedha, jinsi gani ya kuiheshimu fedha

Hapa kuna vitabu vingi Sana vimeandikwa na Hawa jamaa na wana watu mashuhuli duniani ambao wameandika mambo mengi kuhusu upande huuu wa elimu pia Watoto wao wanahamasishwa sana kusoma huku na haya mambo yamewaletea maendeleo Makubwa sana

Ingine ni elimu ya dini pamoja na mambo yote yahusuyo ulimwengu yani vitu Kama kujitambua mwenyewe, utulivu wa akili vitu Kama tahajudi na mengine mengi wametilia mkazo sana ndio mana unaona hata watu wao wanauwezo wa kugundua baadhi ya mambo bila hata kua na elimu hii rasmi

Kwa hapa bongoland sijui Kama kuna muandishi amewahi kuandika kuhusu umuhimu wa tahajudi lakini kule kuna vitabu vingi Sana na vinasidia huku utaambiwa ushaanza shirika sasa

Wakuu hebu tujadili hili kwa muongozo WA haya maswali mawili matatu

1. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kupitia hii elimu rasmi lakini wana vipaji vingi na vinaweza kusaidiwa kwa mfumo ambao sio rasmi je hapa Hakuna namna kabisa ya kuwakomboa Hawa?

2..Teknolojia imebadilika na maisha kwa ujumla yamebadilika wakati elimu rasmi haijabadilika je ni wakati sasa wa kuingiza baadhi ya vitabu visivyo rasmi ili kajaribu kulikomboa taifa?

3. Jinsi gani tunaweza kuingiza elimu ya kujitambua Kama tahajudi(medtation) katika Jamii ili angalau watu wajielewa na wajue kwa nini wapo hapa walipo?

4.Je Hakuna kabisa umuhimu wa hii elimu isiyo rasmi katika jamii?

Natanguliza shukrani sana View attachment The Spirit of Kaizen_ Creating Lasting Excellence One Small Step at a Time_ Creating Lasting E...pdf
 
Back
Top Bottom