Fernando Wolle
JF-Expert Member
- Aug 19, 2022
- 387
- 772
Mko gado humu!? Pole kwa nitakayemgusa moja kwa moja au kupitia mtu wake wa karibu.
Basi Kuna nyakati ukifikiria masuala ya nchi na maamuzi yanayofanywa na viongozi wetu kuhusu mustakabali wa nchi yetu na maisha ya Watanzania unaweza kujiuliza kwamba hivi watu huwa wanapata elimu ili wawe wajinga au ili waisaidie jamii kutatua matatizo?
Sasa nimejaribu kufanya survey ndogo, pengine kama kuna mwingine ana mifano anaweza kuiweka kwenye maoni. Ni kwamba Tanzania ili uonekane wewe kweli umeenda shule huwa kinaangaliwa cheti. Suala la cheti kukifanya kama dhahabu au almasi ndio limefanya watu watumie mbinu zote kukipata.
Kuna watu wengine wana connection za ndugu zao wapo serikalini kwenye vitengo vikubwa sasa kwa bahati mbaya unakuta hana sifa za kielimu, nafasi zinapotokea huwa wanatumia nguvu nyingi sana ili wawekwe kwenye ile sehemu. Watu walibeza sana operesheni ya vyeti feki ya Magufuli lakini ilikuwa ina maana kubwa sana ingawa asingeweza kuwamaliza vilaza wote.
Miaka ya nyuma huko watu wamesomea majina ya watu, watu wamenunua majina, wamenunua vyeti, wamefanyiwa mitihani, wamefaulishwa kwa kulazimisha lengo ni kupata cheti. Matokeo yake ndio haya leo tunayaona, kuna wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, kuna vyeo vingi vya ngazi za juu watu wamepachikwa kule pasipokuwa na mastahili, matokeo yake ndio maamuzi ya hovyo kiasi kwamba kiongozi akifanya maamuzi mpaka raia wa kawaida anajiuliza mara mbilimbili kwamba huyu kweli alienda shule?
Na hata thamani ya elimu imedidimia, elimu imekuwa useless, mtu ana digrii ya kuunga unga kuanzia kwenye mitihani ya sekondari huko kalazimisha wee mpaka kapata cheti, ukizungumza naye utajua tu kwamba hii ni elimu ya kuungaunga.
Maamuzi ya viongozi yanakosolewa vikali kwasababu akili wanazoziongoza ni kubwa sana, ndizo zilistahili kuwa pale. Elimu ni muhimu sana kwenye kusaidia kufanya maamuzi hasa kwenye masuala ya nchi na uongozi wowote, lakini kuna uwezekano mkubwa sana menejimenti za maamuzi zilizo nyingi ziliingia hapo zilipo kutokana na kulazimisha sana elimu na upendeleo.
Kuna watu hutetea kwamba uongozi ni Karama, Uongozi ni Kipaji na kwamba elimu sio suala la muhimu sana katika uongozi, huu mimi nauita ni upuuzi na kama tutaendelea kuwa na mtazamo huu basi tutakesha sana kama nchi kufikia hatua ya kujitegemea kiuchumi.
Elimu ambayo haijaghushiwa ni muhimu sana sana katika masuala ya uongozi, achana na elimu za viongozi ambao wamesomea majina ya watu, wamenunua vyeti, wamerudia na kurudia na kurudia ili tu apate credit za kupata cheti.
Elimu ni muhimu lakini usiilazimishe kama imekukataa. Elimu ikikukataa soma hata elimu ya maarifa tu ya kufanya mambo yako mengine ya kuendesha maisha yako binafsi sio kulazimisha kuwa mwanataaluma kwa kununua cheti, kufanyiwa mtihani, kununua jina au kurudia na kurudia na kurudia nakurudia tena na tena. Utalazimisha lakini ombwe litaonekana tu.