Elimu: Hoja sio ubovu wa mkataba bali hoja ni wizi unaofanywa na muwekezaji!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,155
29,677
Kwa muda sasa tunaona wanojiita wapinzani au wajuawaji wa sheria eti tutapata hasara au Rais amekosea.

Hoja ya msingi iliyopelekea Rais kuteua tume ya kufuatilia ni kipi tunachopata kwenye mkataba uliopo wa madini ni kutaka kujua kama tunapata kile ambacho kwa kilichosemwa na mkataba ?

Hadidu za rejea kwa tume ziko wazi kabisa na tume imetoa ripoti ya wazi kabisa.

Sasa kuna wanasiasa uchwara wanataka kutuondoa kwenye hoja ya msingi.

Sijaona sehemu Tume ikijibu au kuagizwa kuwa mkataba ni halali au sio halali ?au mkataba ni wa kipuuzi au la...pengine tume ya pili inaweza kujibu hili!!

leo hii tumeelezwa kuhusu wizi unaotokea ndani ya mkataba ambao unaweza kuwa ni wa kinyonyaji au la.

Hoja ya msingi ni je katika mkataba huo huo tunaoushupalia je tumeibiwa au la.

Inawezekana kabisa by the time mkataba unaingiwa kulikuwa na maslahi ya kuweza kutuneemesha...lakini wakati wa utekekezaji mwekezaji akatumia rushwa na ujanjaujanja kutuibia.

Kwa hiyo hoja ya kujadili ni wizi ndani ya mkataba.

Prof Mruma ametufumbua macho kwamba tunaibiwa...tusikubali mwanavarangati aliyesomeshwa na kodi zetu na kupewa rushwa na wawekezaji kutudanganya.

Twende step by step!Tutulize mshono..tujadili wizi ndani ya mkataba halafu ndio tutajadili ubovu wa mkataba(tume ya kisheria itatuambia)

Tutamuelewa tu Mh.Rais!
 
"..serikali haijawachukulia
hatua zozote kampuni yoyote
ya madini au mwekezaji
kutokana na ripoti ya
makinikia. Kwamba hatua
zilizochukuliwa ni za ndani tu
haxiwahusu hao
wawekezaji. Hivyo
wasiwe na wasiwasi na
waendelee na shughuli
zao kama kawaida. Lengo
la serikali ni.kujiridhisha
tu kilichopo kwenye
makinikia..."
Kasim Majaliwa Kasim.
Waziri Mkuu
01/06/2017
WM wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo leo Bungeni!
 
"..serikali haijawachukulia
hatua zozote kampuni yoyote
ya madini au mwekezaji
kutokana na ripoti ya
makinikia. Kwamba hatua
zilizochukuliwa ni za ndani tu
haxiwahusu hao
wawekezaji. Hivyo
wasiwe na wasiwasi na
waendelee na shughuli
zao kama kawaida. Lengo
la serikali ni.kujiridhisha
tu kilichopo kwenye
makinikia..."
Kasim Majaliwa Kasim.
Waziri Mkuu
01/06/2017
WM wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo leo Bungeni!
yap..ni ukichaa wa wawrkezaji na wapibzani vigeugeu kudhani kwamba serikali imemgusa muwekezaji ...badi ripoti ya hayo tunaisubiria
 
"..serikali haijawachukulia
hatua zozote kampuni yoyote
ya madini au mwekezaji
kutokana na ripoti ya
makinikia. Kwamba hatua
zilizochukuliwa ni za ndani tu
haxiwahusu hao
wawekezaji. Hivyo
wasiwe na wasiwasi na
waendelee na shughuli
zao kama kawaida. Lengo
la serikali ni.kujiridhisha
tu kilichopo kwenye
makinikia..."
Kasim Majaliwa Kasim.
Waziri Mkuu
01/06/2017
WM wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo leo Bungeni!
Aangalie asijekutana na barua kesho
 
Raisi alisema alisema ukiona watu watoa povu kutete wizi ujue una kik
Lisu na genge lake ni kik
 
yap..ni ukichaa wa wawrkezaji na wapibzani vigeugeu kudhani kwamba serikali imemgusa muwekezaji ...badi ripoti ya hayo tunaisubiria
Hasara wanayopata hujaiona?Vp ikigundulika tulikuwa wrong,uko tayari kuwafidia!
 
These people you are slighting are your kingmakers. Let's see if they will still pick you to rule this fiefdom when you are not toeing their line.
 
Kusema tunaibiwa bila kujua ni shs ngapi tunaibiwa naona ni sawa na wivu wa kimapenzi,

unatuhumiana kwa ushahidi wa kimazingira tu bila kuwa na uhakika. Lisu nae kawa pumbafu tu, sasa tuache kuchunguza kisa mzungu?
 
  • Thanks
Reactions: kg1
Dah!
Inauma sana. Tena sana yani zaidi ya sana.

Nilishaachaga kitambo sana kufuatilia mambo ya siasa. Ila kwa hili la rais wa TLS, Mheshimiwa Tundu Lissu limenishinda kuvumili.

Hebu msikilizeni anachosema mwanasheria huyu kuhusu kukamatwa ule mchanga wa dhahabu, huenda labda nyie wenzangu mtakuwa mmemuelewa then. Aliyemuelewa nae atanijuza ili na mimi nimuelewe kama alivyomuelewa yeye.

Na hapa namnukuu;

"Tanzania ni mwanachama wa kitu kinachoitwa the Mager Convasion. Mager ni mult vatral investment garanty agency wa Benki Kuu ya Dunia. Ukiwa mwanachama, wawekezaji wakileta mali zao kwako kisha ukachukua mali zao kama alivyochukua Magufuli namna hii, utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko.

Tunasaini mikataba ya ulinzi wa wawekezaji na mataifa ya wanapotokea wawekezaji hao ambayo ni Marekani, Canada, England nk. Wote hao ni mabosi wakubwa.

Makampuni ambayo Magufuli anayakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi.

Tuna by eletro investment treates ambazo zinalinda mikataba yao.

Rais wetu kama kawaida yake,
Anashaurika?
(hapana ye huwa hangoji ushauri)
Sasa amejiingiza kwenye mgogoro mkubwa".

Mwisho wa kumnukuu.

Dah!
Kwa mimi mwananchi wa kawaida imeniuma sana kumwona rais wa wasomi wote wa sheria Tanzania akiongea maneno haya, huku nikijiuliza maswali ambayo sijapata majibu. Labda mje mnijuze wenzangu.

1. Mheshimiwa Lissu unaposema (mali zao walizokuja nazo)
Ni zipi hizo?
Wakati wao ndo wamekuja kutafuta mali huku kwetu?

2. Mheshimiwa Lissu mikataba tuliyosainiana nao hao jamaa, inasema chochote watakachokipata katika uchimbaji wao, basi wasiulizwe wamepata kiasi gani?

3. Mheshimiwa Lissu iwapo wawekezaji wametuambia eti wamepata dhahabu tani 3 baada ya uchunguzi tukagundua wamechimba tani 7, hapa aliyekiuka mkataba ni yupi kati ya mwekezaji na serikali husika?

Daa!
Hapa nimekwama kupata majibu kwakuwa mimi sikusoma, lakini hata kuona pia nisione jamani?

Daah!
Inauma sana
Tena sana
Kuliko hata sana.
 
hivi umelielewa hilo tamko la waziri mkuu?
Ameelewa,ametuma msg kuwa watu wasitishike na maneno ya Rais day 1,kile kilikuwa kikao cha ndani cha serikali na wala hakina madhara kwa kampuni ya ACASIA,waendelee na uchimbaji bila wasiwasi!
 
Kusema tunaibiwa bila kujua ni shs ngapi tunaibiwa naona ni sawa na wivu wa kimapenzi,

unatuhumiana kwa ushahidi wa kimazingira tu bila kuwa na uhakika. Lisu nae kawa pumbafu tu, sasa tuache kuchunguza kisa mzungu?
Mfumo wa elimu tanzania ni wa ovyo sana (kama umesoma tanzania)
Kama kujenga hoja unatoa boko namna hii
 
Inawezekana hatusikilizani au hatujui hata tunachozungumza; au wote tunazungumza ya Kweli Ila hatujui kwa kuwa hatusemi mambo ya msingi ya nchi hii. Sasa tunawaona Watu badala ya hoja wanazosema!
 
Namwelewaga Sana huyu Jamaa anayeitwa Tundu Antipas Lissu. Msomeni hapa wenyewe;

"ANAANDIKA TUNDU LISU...

....Suala sio nia njema ya Rais. Suala ni consequences za hiyo nia njema. The road to hell is paved with good intentions.

Mugabe most likely alikuwa na nia njema. The consequences za nia njema hiyo ni kwamba Zimbabwe ya leo haina hata sarafu yake na imegeuka kuwa ya kuomba chakula wakati ilikuwa a major food exporter.

Kama kweli Rais Magufuli ana nia njema angeanza na mfumo mzima wa kisheria, sio kuhangaika na magwangala.

100% ya uzalishaji wa dhahabu ya Geita unafanyikia mgodini na Geita Gold Mine ni mgodi mkubwa kuliko yote nchini.

Kwa logic ya Magufuli ni kwamba GGM hawatuiibii kwa sababu tu smelting yote inafanyikia Geita.

Acacia wanayeyushia dhahabu yote ya Nyamongo mgodini Nyamongo.
Kwa logic hiyo hiyo, hawa wezi wa mchanga wa Bulyanhulu na Buzwagi hawaibi Nyamongo kwa sababu tu wanafanya kila kitu Nyamongo.

Resolute walisafisha 100% ya dhahabu yao Nzega mpaka walipokomba kila kitu na kuacha mashimo na maji ya sumu tu.

Kwa logic ya wazalendo wetu, hatukuibiwa Nzega kwa sababu wawekezaji hao hawakusafirisha mchanga wa dhahabu.

Acacia walishakomba kila kitu Tulawaka na kuacha mashimo na maji ya sumu. Kwa sababu tu hawakusafirisha mchanga, basi hawakuwa wezi.

Hii ni logic ya mtu asiyeelewa biashara ya uchimbaji dhahabu katika nchi hii kabisa.
Tangu tumeanza kuwakaribisha wawekezaji hawa, hatujawahi kufikisha 10% ya mapato ya kikodi kutokana na mauzo ya dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje.

Sio kwa sababu wawekezaji walikuwa wana-underdeclare mchanga wa dhahabu, bali ni kwa sababu sheria zetu zinawaruhusu kutokulipa kodi kama hawajatangaza faida.
Ni sheria, sheria, sheria. Sio mchanga wa dhahabu. Hilo ni changa la macho tu la kufumbia wasioelewa.

Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema.
Mnaambiwa tusiogope kushtakiwa. Munatiwa ujinga na hao hao waliowaruhusu wageni kuchota mali zetu: akina Magufuli na CCM yao.

Tumeshalipishwa na tunaendelea kulipishwa mabilioni mengi kutokana na kesi za Richmond/Dowans, IPTL/Tegeta Escrow, City Water, Samaki wa Magufuli, n.k. kwa sababu tumekuwa tunakiuka mikataba 'kwa nia njema.'

Tumekuwa tunaingia hasara kubwa kama taifa kwa sababu za kijinga. Badala ya kukataa ujinga huu tunaushabikia kwa sababu tu umefanywa 'kwa nia njema.' Magufuli atauachia huo mchanga wa dhahabu kwa wenyewe. Mark my words. Hana jinsi.

Sheria yetu ya madini inasema huo mchanga ni mali yao. Na imesema hivyo tangu mwaka '98.
Mkataba wao unasema ni mali yao. Na umesema hivyo tangu mwaka 2000.
Mikataba ya kimataifa tuliyosainishwa na wenye nia njema hawa inasema mchanga ni mali ya Acacia.

Mchanga huo umehakikiwa na TRA, TMAA, GST na SGS. Zote hizi ni taasisi za Serikali hii hii na zimepewa mamlaka kisheria na kimkataba na Serikali hii hii kuhakiki mchanga huo.
Kamati ya Prof. Mruma haina mamlaka hayo. Ripoti yake haina maana yoyote kiushahidi.
Sio kupiga ramli au kuagua kusema kwamba tutapigwa asubuhi kwenye arbitral tribunals za kimataifa.

Tutawarudishia mchanga na tutawalipa hasara yote waliyopata kwa sababu ya matendo yenye nia njema lakini yasiyozingatia sheria wala busara katika mambo haya.

Tunarushiwa changa la macho lingine. Tunaambiwa kuna Kamati ya wachumi na wanasheria inaleta ripoti nyingine. Hii itakuwa Kamati ya nne tangu mwaka 2004. Tulikuwa na Kamati ya Dr. Jonas Kipokola (2004); Lau Masha (2006) na Jaji Mark Bomani (2008). Tumekuwa na taarifa lukuki za watafiti binafsi na kwa muda mrefu. Ni kitu gani hasa cha kiuchumi au kisheria ambacho hatukijui hadi sasa na ambacho kinahitaji kuundiwa Kamati nyingine??? Wajinga ndio waliwao. Mimi sio mjinga. Na sijahongwa kama hawa wanajiita wazalendo. Ninapinga na nitaendelea kupinga ujinga huu unaotupeleka kuzimu......" Tundu Lisu

Soma hiyo hapo utamwelewa.
 
Back
Top Bottom