Ni sera mbovu za CCM. Hili aliliongelea Dr Slaa pale jangwani, ambapo alishangaa kwamba serikali ya JK eti imetoa ajira za watu milioni 1.3 katika miaka yake mitano! Dr Slaa alisema kuna vijana wana degree za chuo kikuu wanatembea nazo mfukoni hawana kazi, jee ni ajira gani hizo JK anajigamba nazo? Umachinga? Kwani nchi hii imekuwa condemned kuwa a nation of machingas? Yaani serikali haina mkakati mwingine wa kutoa ajira? alishangaa Dr Slaa.