Elimu Bure;shida tumezoea mteremko

Viva89

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
1,261
526
wapendwa, habari zenu

nimeangalia habari sasa hivi ITV nimekutana na habari ya wananchi kule Bagamoyo sijui kijiji gani wakilalamika na kusema hawatawapeleka watoto wao shule kwa kuwa shule imewaambia watoe mchango wa laki mbili (200,000) kwa ajili ya chakula cha watoto na kwamba Rais alisema elimu ni bure kuanzia Januari. Wakaelezewa jinsi hiyo sheria ya elimu bure ilivyo na wananchi wamesema sasa hiyo sheria ya elimu bure inawasaidia nini?

Naelewa, laki mbili ni ndefu kwa maisha ya kijijini, ila inakuwaje mtu ukiambiwa elimu bure ndio unajua mzazi unakaa pembeni kwenye masuala ya fedha ya aina yoyote juu ya mtoto?! tutaishia kuipa serikali mzigo mzito sasa.
Shida ganda la ndizi.
 
Elimu bure ina tafsiri nyingi. Mfano enzi za mwalimu Nyerere ilimaanisha ufundishaji, vifaa vya shule km daftari na hata chakula. Sasa elimu bure ya sasa inaweza kuwa tofauti. Ni vizuri wananchi waelezwe na wanasiasa tafsiri ya sasa ya elimu bure. Bila hivyo italeta shida kwa wafanyakazi wa idara ya elimu na hasa waalimu.
 
Back
Top Bottom