Ntigy
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 489
- 267
Pengine serikali ina nia njema,lakini imeshindwa kujipanga kwanza badala yake suala hili limepelekwa kwa mihemko ya kisiasa. Serikali inatoa fedha zilizokuwa zikilipwa kwaajili ya ada ya shule, lakini wamesahau kuwa shule zilikuwa zinaendeshwa na zaidi ya ada. Kulikuwa na michango mbalimbali kama ya taaluma,ulinzi,maji,ukarabati,n.k. michango hiyo ilikuwa inasaidia sana uendeshaji wa shule.
Ukosefu wa michango hiyo kwa sera ya ELIMU BILA MALIPO imekuwa mateso bila chuki:-
Wadau wa elimu iangalieni upya hii sera ya elimu bure,bado ina changamoto nyingi!
Ukosefu wa michango hiyo kwa sera ya ELIMU BILA MALIPO imekuwa mateso bila chuki:-
- Hakuna fedha za kuchapia mitihani,hivyo walimu wanaandika mitihani ubaoni.
- Fedha hazitoshi kununulia vitendea kazi,hivyo walimu wanalazimika ama kujinunulia vitendea kazi au kutumia maarifa ya ziada.
- Walinzi na wahudumu wa shule wanalazimika kukaa miezi kadhaa pasipo kulipwa mishahara.
- Baadhi ya wanafunzi hawana madawati ya kukalia,hivyo wanalazimika kushare kiti kimoja wanafunzi wawili.
- Wanafunzi wanalazimika kuchana madaftari yao ili kuandikia mitihani kwasababu shule hazina karatasi za rimu.
Wadau wa elimu iangalieni upya hii sera ya elimu bure,bado ina changamoto nyingi!