Elimu bure ikigoma, ifanyike kama elimu ya juu mzazi alipe kulingana na uwezo wake

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
407
607
Kuna kila dalili kuwa mpango wa elimu bure utagoma, hali ya shule zetu zitakuwa mbaya hasa kwenye miundo mbinu, fedha inayotolewa haitaweza kutengeneza hata madawati kama haitatolewa kwa mikupuo hata ya miezi mitatu mitatu au minne.

Ushauri wangu serikali iachane na mpango huu wa hata aliye na uwezo kusomeshewa mtoto wake bure badala yake, mtu alipe kulingana na uwezo wake kama ilivyo kwa elimu ya juu.

Kwa nchi inayoendelea kama Tanzania haileti afya kwa wakulima wakubwa , watumishi wa serikal, taasisi na makampuni, wafanya biashara wakubwa kulipiwa ada isiyozidi hata laki moja kwenye shule za sekondari za kata. Setikali ingewatoa katika mpango huu makundi haya.

Na fedha zitakazookolewa zikaelekezwa kulipa madeni ya watumishi, kukamilisha maabara, kununua vyombo vya usafiri vya shule, kujenga vyoo, nyumba za walimu n.k. Lakini serikali kwa kutaka kuwasaidia makundi ya wazazi ada za shule watu wenye uwezo wa kulipa ada itashindwa kuimarisha huduma za miundo mbinu na kuboresha mahitaji ya walimu.

Kwa mfano kama ikisema wazazi wajilipie wenyewe ada ya mtihani Tsh 50,000 ya kidato cha nne nchi nzima, na kidato cha pili Tsh 10,000 kwa nchi nzima.

Fedha hizi ambazo zingetumika kulipia mitihani zikatumika kulipa walimu madeni yao inaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa kama siyo kumaliza kabisa kero ya madeni ya walimu na kuinua ari ya walimu wetu.

Kwa kuwaangalia wazazi na kuwatelekeza walimu tusitengemee ubora wa elimu hapa.
 
Last edited by a moderator:
Ikishindikana ina maana mtu kashindwa. Ahadi za majukwaani hazitekelezeki!!
Kiasi cha fedha kinachotolewa ni kiduchu mno, na mwanzo wa muhula mahitaji ni makubwa mno. Viongozi wa Elimu hawamwambii ukweli JPM. Subiri waandishi watembelee shule. Wazazi walilipa pesa nyingi kuliko serikali.
 
Mimi ni mwl.Leo tumekaa siku ya tano tunajadiri pesa ambayo wala haifiki milioni moja.Walimu tunaumiza vichwa kupiga bajeti,pesa kidogo mahitaji mengi.Mpango huu umeishashindwa!!
 
Mimi ni mwl.Leo tumekaa siku ya tano tunajadiri pesa ambayo wala haifiki milioni moja.Walimu tunaumiza vichwa kupiga bajeti,pesa kidogo mahitaji mengi.Mpango huu umeishashindwa!!

Wamuulize LOWASA ............ Waliposikia Lowasa anasema ELIMU, ELIMU, ELIMU wakacopy. Kama kweli Lowasa alikuwa na mkakati na si kutafuta kura basi awaambie namna ya kufanikisha hili la elimu bure mpaka University.

By the way, laptop zimekwishawafikia!!?
 
Back
Top Bottom