Mpangawangu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2014
- 887
- 965
Elimu bure na Changamoto zake.
Kwanza naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kupanga na kutekeleza sera ya Elimu Bure.
Pamoja na kuwa mpaka sasa karibu shule zote zimeshaingiziwa fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule bila kumchangisha mnyonge wa Tanzania.
Ni vyema tukatambua kuwa awali kabla ya serikali kuanza kutekeleza sera hii ya Elimu bure wazazi walichangia katika maeneo yafuatayo.
1.Wazazi walichangia gharama za kumuandikisha mtoto shule
2.Mchango wa dawati(Kiti na Meza)
3.Gharama za uchapishaji wa mitihani(Mitihani ya wiki,Mwezi,Muhula)
4.Gharama za kuwalipa walimu wa kujitolea(Part time teacher)hasa kwa masomo yasiyo na waalimu kama vile Physics,Chemistry ,Mathematics ,Book-Keeping na Commerce.
5.Mchango Mlinzi(Shule nyingi zina walinzi wawili)
6.Shule za Sekondari zina Mchango wa secretary kwaajili ya kumsaidia mkuu wa shule .
Hiyo ndiyo michango iliyogeuka kuwa kero kwa watanzania Maskini wanaowasomesha watoto wao kwenye shule za serikali.
Sasa bila ushabiki wowote usio kuwa na tija kwa nchi tujadiliane pamoja kiasi cha fedha kilichotolewa na serikali ili kuubeba mzigo uliokuwa unabebwa na Wananchi wanyonge wa Tanzania.
Kwanza ni ukweli usiofichika kuwa zipo gharama zinafanana hata kama shule zinatofautiana idadi ya wanafunzi.
Kila shule lazima iwe na gharama za kuwalipa wakinzi bila kujali idadi ya wanafunzi.
Kila shule inaouhitaji wa madawati.
Fedha iliyotolewa na Serikali pamoja na kuwa ni kidogo sana kwa shule,serikali imeweka mchanganuo ambao umeacha mambo muhimu ya kuhojiwa na kila mwenye fikra huru.
Kwenye mchanganuo uliotolewa na serikali hakuna ambapo serikali imeonyesha madawati ya wanafunzi yatanunuliwa kwa gharama gani .
Hakuna mtoto anaeweza kujifunza bila kuwa na mazingira bora ya kujifunzia,majibu mepesi yanayotolewa na baadhi ya wananchi ni kuwa watoto wa form one watatumia madawati ya kaka zao waliomaliza form four.
Ukweli ni kuwa zipo shule nyingi tu hazijawahi kuwa na wahitimu wa form four.
Maana yake kila mtoto atatumia dawati alilonumuliwa na Mzazi wake,Je hao wapya walioambiwa wazazi wasichangie dawati watatoa wapi madawati?
Pia hata shule ambazo zimeshapata wahitimu,Madawati mengi yaneshaharibika,kuna idadi kubwa ya viti visivyotengenezeka tena,hata vilivyopo haviwatoshi wanafunzi tofauti na wengi wanaoamini kuwa viti huwa vinauzwa na wakuu wa shule.
Nikirejea kwenye mahitaji mengine,Eneo la Mitihani limetengewa asilimia 15% ya fedha yote ya Elimu bure.
Kwa shule yenye wanafunzi 200 tu ,halafu ikapewa shilingi laki tatu za kuendeshea shule kwa mwezi maana yake 15% ya laki tatu ni sawa na Sh.45000/= yaani utumie shilingi 45000 kununua rim za kuendeshea shule,pamoja na kuchapisha mitihani ya kila wiki na kila mwezi.
Naona kama muujiza ,labda ma jenious wa Hesabu wataweza kuchapisha mitihani ya watoto 200 kwa shilingi 45000.
Mchanganuo nambari moja unamtaka mkuu wa shule kutumia 35 ya fedha zote kwaajili ya Kumlipa Mlinzi,Kununua Mashajara,kununua maandalio,Kulipa bili ya maji na kulipia umeme kwa shule zenye umeme.
Hebu tutumie mfano wetu hapo juu wa shule yenye watoto 200 iliyojipatiaa kitita cha laki tatu.
Asilimia 35 ya laki tatu ni sawa na Sh.105000(laki moja na elfu tano)
Kuwa Mkuu wa Shule anapaswa kutumia laki na elfu tano kuwalipa walinzi wawili wanaolipwa sh.80000 kila mmoja (Chini ya kima cha chini cha serikali),kulipia bili ya maji(Mnajua matumizi ya maji kwa wanafunzi) ,kulipia umeme,kununua mashajara na Maandalio,pamoja na kutumia 10% ya laki na elfu tano kwaajili ya kuendeshea shule nauli ya mkuu wa shule anapofuatilia jambo Ofisini.
Ni Mtu tu aliepata A+ ya Hesabu anaeweza kuzitumia hizo fedha akafanikiwa kuendesha shule.
Hatari kuliko yote ni swala la walimu wakujitolea ambao ndio wakiowasaidia watoto waliosoma shule zetu walau kupata div four.
Shule nyingi hasa za vijijini hazina walimu wa kutosha hasa kwenye masomo ya Sayansi,Biashara na Hisabati.
Wakuu wengi wa shule waliwatumia vijana waliomaliza kidato cha sita wanaosubiri post za vyuoni kuwasaidia vijana huku wakilipwa kati ya laki moja mpaka laki mbili.
Fedha hizi zilichangiwa na wazazi ili watoto wao wasikose masomo muhimu.
Katika Mwongozo uliotolewa hakuna upenyo wowote wa kuwatumia maana hakuna hata mia kwaajili ya kuwalipa.
Kwa lugha rahisi ni kuwa wakuu wa shule hawatawatumia tena,sasa hapa ndipo panatisha hasa kwa watoto wa vijijini.
Naishia hapo kwa leo lkn naziona dosari kubwa katika utekelezaji wa sera hii.
Karibuni tujadiliane hasa tukilenga kunusuru hali kama walivyonusuriwa watu waBomoa Bomoa