Elimu bure chanzo cha matatizo yote awamu ya 5

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Wakuu,

Utawala wa awamu ya tano ulianza kwa mbwembwe nyingi na sera za kukurupuka bila hata ya kuzifanyia utafiti wa kutosha juu ya utekelezwaji wake na zitaathiri wizara sekta na sera zingine.

Ni wazi sera ya elimu bure ndio kiini cha matatizo mengi kwa sasa nchini, miradi mingi inakwama kwa pesa zake kupelekwa kukamilisha elimu bure. Ajira mpya hakuna sababu pesa imepelekwa elimu bure. Marimbikizi na kupanda madaraja kwa wafanyakazi hakuna, pesa imepelekwa elimu bure!

Dawa hospitali hali tete pesa iko elimu bure.Walimu hali mbaya, makato ya loan boad sababu ni elimu bure

Sio kwamba napinga sera ya elimu bure, ila serikali na tanzania kwa ujumla tulikuwa bado tujajipanga na hatutoshi kuitumikia elimu bure!

Mtukufu rais, elimu bure ndio chanzo cha shida zote hizi
Jaribu kuipitia upya sera hii na uje na uamuzi mgumu kuipiga marufuku ili nchi irudi kwenye hali yake na mambo mengine yaendelee.
 
hiyo elimu bure unayosema inaishia form 4 .... bado haupo sahihi ila chanzo cha matatizo ni kutumia pesa nyingi kwenye makorokoro bila kuangalia wananchi wako wanaishije....
1. ununuzi wa ndege..
2. kuhamia dodoma
3. ujengaji wa barabara za juu

sasa hayo yote yafanywe kwa muda mfupi.. kwann hali isiwe tete... na hashauriki sasa..!!!
 
Watu walishazoeshwa tangu enzi ya mwinyi kuchangia gharama .....wakazoea,kuanzia msingi mpaka "A" level,chuo wakopeshe kwa bodi ya mikopo,inakuja unafanya kinyume,ile elimu ya msingi mpaka A level ambayo mzazi anamudu,unamwambia bure,ile asiyoimudu ya chuo kikuu,unalazimisha ajigharamie,na unakatakata mikopo,

Hivi kuna mzazi anashindwa kuchangia elfu kumi shule za msingi au hata 20?

Je ni wangapi wanaweza kulipa mamilioni ya chuo kikuu?

Matokeo yake unakata fungu la chuo kikuu ugharamie elimu ya msingi

Au unakata fungu la ajira ugharamie shule za msingi/sekondari,hela yenyewe kwa kila shule,unapeleka laki moja mbili,inunue chaki,mlinzi,maji,umeme,........

Katika ngazi ya chini kabisa TUNAWAZOESHA watanzania waiulize nchi inawafanyia nini,sio wao wanaifanyia nini,walizoea kuifanyia nchi kuchangia elimu,sasa tumewarudisha miaka 30 nyuma wanaanza kuuliza nchi inawanyia nini
 
hiyo elimu bure unayosema inaishia form 4 .... bado haupo sahihi ila chanzo cha matatizo ni kutumia pesa nyingi kwenye makorokoro bila kuangalia wananchi wako wanaishije....
1. ununuzi wa ndege..
2. kuhamia dodoma
3. ujengaji wa barabara za juu

sasa hayo yote yafanywe kwa muda mfupi.. kwann hali isiwe tete... na hashauriki sasa..!!!
Hata hapo kwa form 4 si pakubeza mkuu.......mleta mada ana point muhimu, ni kweli pamoja na hizo ndege na uhamisho wa kwenda Dodoma, lakini bado hela ndefu inagharamia elimu bure, na hii Sera itatutoa roho wallah......nadhani mheshimiwa alirukia kibwagizo cha Lowasa bila kujua mwenzake alijipangaje.
 
Walidandia hii sera kutoka upinzani ili washinde but haikuwa katika malengo yao so walikuwa hawajipanga kabisa. So wanajitutumua huku wakifa na tai shingoni
 
hiyo elimu bure unayosema inaishia form 4 .... bado haupo sahihi ila chanzo cha matatizo ni kutumia pesa nyingi kwenye makorokoro bila kuangalia wananchi wako wanaishije....
1. ununuzi wa ndege..
2. kuhamia dodoma
3. ujengaji wa barabara za juu

sasa hayo yote yafanywe kwa muda mfupi.. kwann hali isiwe tete... na hashauriki sasa..!!!
Wakati nchi INA shida ya maji, watumishi hawana ongezeko la mshahara wala kupanda daraja,watumishi hawalipwi madeni,mawakala wa pembejeo hawajalipwa na Mali zao zinakaribia kuuzwa,wakandarasi madeni yao yanahakikiwa kila siku bila kulipwa,

Kuna mtu atatenga matrilioni kujenga maghorofa dodoma(wakati mengine kayaacha Dar mapyaaaa)atatenga matrilioni kuhamisha maelfu ya watumishi waende dodoma,atatenga mabilioni kununua fenicha,kukodi maofisi,

Kisa? Anataka tu kuhama!

Wanafunzi hawana mikopo,akina mama wanabeba ndoo za maji kichwani hakuna maji ya bomba... Lakini mtu tu kaamua kuhama

Bukoba hawana meli ya kama walivyoahidiwa.....tumeamua kuhama.....

Mimi si mchumi,lakini najua Dodoma ni kaburi la hela,zitazama na hazitaleta faida.

Wizara ya maliasili jengo lao jipyaaa hata halina miaka mitano,unawaambia waliache,waende dodoma wakapange ofisi na baadae wajenge tena!!

Sielewe
 
Elimumsingi = Darasa la kwanza hadi kidato cha nne = Elimu bure

Hapa ndipo pesa nyingi inatumika pasipo na tija yoyote kwa maana ya kuwa ufaulu ni uleule au mbovu zaidi. Shikamoo elimu bure
 
Elimumsingi = Darasa la kwanza hadi kidato cha nne = Elimu bure

Hapa ndipo pesa nyingi inatumika pasipo na tija yoyote kwa maana ya kuwa ufaulu ni uleule au mbovu zaidi. Shikamoo elimu bure
Nadhani ukifanyika utafiti ambao si wa wale Hakielimu, muda wa miaka michache ijayo elimu itakuwa hovyo pamoja na miundombinu

Haki elimu tafiti zao huwa "zinatekwa" kabla hawajazitoa wazi pale habari Maelezo kwa harmomwake
 
Wakati nchi INA shida ya maji, watumishi hawana ongezeko la mshahara wala kupanda daraja,watumishi hawalipwi madeni,mawakala wa pembejeo hawajalipwa na Mali zao zinakaribia kuuzwa,wakandarasi madeni yao yanahakikiwa kila siku bila kulipwa,

Kuna mtu atatenga matrilioni kujenga maghorofa dodoma(wakati mengine kayaacha Dar mapyaaaa)atatenga matrilioni kuhamisha maelfu ya watumishi waende dodoma,atatenga mabilioni kununua fenicha,kukodi maofisi,

Kisa? Anataka tu kuhama!

Wanafunzi hawana mikopo,akina mama wanabeba ndoo za maji kichwani hakuna maji ya bomba... Lakini mtu tu kaamua kuhama

Bukoba hawana meli ya kama walivyoahidiwa.....tumeamua kuhama.....

Mimi si mchumi,lakini najua Dodoma ni kaburi la hela,zitazama na hazitaleta faida.

Wizara ya maliasili jengo lao jipyaaa hata halina miaka mitano,unawaambia waliache,waende dodoma wakapange ofisi na baadae wajenge tena!!

Sielewe
ahsante mkuu kwa kuweka bayana...
 
Wengi sidhani kama wanalitafakali hili ila upo sahihi kabisa mengi yatakwama sababu ya elimu bure
 
hiyo elimu bure unayosema inaishia form 4 .... bado haupo sahihi ila chanzo cha matatizo ni kutumia pesa nyingi kwenye makorokoro bila kuangalia wananchi wako wanaishije....
1. ununuzi wa ndege..
2. kuhamia dodoma
3. ujengaji wa barabara za juu

sasa hayo yote yafanywe kwa muda mfupi.. kwann hali isiwe tete... na hashauriki sasa..!!!

Serikali haijatumia pesa yake kujenga flyovers
 
Back
Top Bottom