Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,582
Waungwana naamini hamjambo.
Kama kweli tunapenda watoto wetu wapate elimu inayofaa, tujitoe kutembelea shule wanazosomea. Nimetembelea shule ...... tofauti jijini .... nimekuta vyoo vimejaa, na nilipouliza wahusika wakanieleza kwamba wametoa taarifa miezi mitatu iliyopita lakini hakuna kinachoendelea. Niliwauliza walikuwa na utaratibu gani kwa kipindi cha nyuma, wanadai walikuwa wanawashirikisha wazazi wenye watoto shuleni hapo wanachanga hela na kukodi gari la kuhamisha uchafu huo. Kwa sasa hawana utaratibu huo kwa kuwa elimu ni BURE ... BURE KABISA.
Wanafunzi waliofanya mtihani wa term ya kwanza wengi wameambulia '0' - shida ni kwamba walimu wa kujitolea waliokuwa wakilipwa hela toka kwenye michango ya wazazi hakuna tena.
Form II na IV walikuwa na utaratibu wa kubaki mashuleni kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya Taifa; walimu waliokuwa wanaendelea nao kwa muda wa ziada walilipwa kutokana na fedha zilizochangwa toka kwa wazazi ... kwa sasa hiyo programme hakuna tena kwa sababu elimu ni BURE .. BURE KABISA.
Ninaloliona ni kupata matokeo ya elimu BURE ...BURE KABISA. Tusubilini matokeo ya mwaka huu kwa O level yatakavyokuwa ya kusikitisha ...
Ombi! Kama una mtoto anasoma shule za kata ... fanya hima mtafutie msaada binafsi ili uweze kumnusuru na ELIMU BURE .. MATOKEO BURE.