binafsi kufundisha mda wa likizo ni lazima nilipwe mshahara wa mwezi huo kama posho vinginevyo tutatoana roho
Bora nikalime karanga kulko kufanya kazi ya ualimu
Hasa miwalimu ya shule ya msingi, ni mioga sana, tatizo nadhan ni vyeti vyao
Hasa miwalimu ya shule ya msingi, ni mioga sana, tatizo nadhan ni vyeti vyao
Wakuu hivi ELIMU bure bila kuwajali walimu kweli lengo litafikiwa?
Watz wanafurahishwa na kauli hii lakini je wanajua faida na hasara za ELIMU bure? Kwa taarifa ya uhakika niliyo nayo walimu wa Mwanza jiji katika shule za msingi wamelazimishwa na Afsa elimu kufundisha bure madarasa ya la pili, nne na saba wakati wa likizo.
Hii ni kutekeleza agizo la ELIMU bure,je, walimu hao watakaofundisha madarasa hayo hawana haki ya kupumzika/kukaa likizo baada ya kufanya Kazi mwaka mzima?
Achilia mbali likizo,acha wafundishe, je,kwakuwa ni muda wa ziada hawana haki ya kulipwa posho za kufundisha kipindi cha likizo?
Huku siyo kuwaonea walimu? Walimu HAWA watafundisha kweli kwa dhati? Nahisi Afsa ELIMU Huyu atakuwa amekiuka haki za walimu.
Ndo ivyo walimu baadhi ya miezi mishahara hatujalipwa
Acha kulalamika we ticha uchwara, hiyo ni likizo ya wanafunzi na sio wafanyakazi. Mwalimu ana likizo moja tu kwa mwaka ambayo unapewa hadi nauli.
Una uhakika na unachokisema ati Mimi ni "Mwalimu uchwara?"Asante mkuu kwa kumwerewesha,binafsi nachukia watu wanaopenda kulialia,mi mwenyewe mwalimu naipenda kazi,napenda kuitwa mwalimu mpaka mke wangu nishamzuia kuniita honey,dear sweet,huwa ananiita mwalimu tu.