Mtanzanite
Member
- Jun 18, 2013
- 29
- 2
Madudu zaidi yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya kuwapanga baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano kwenye shule ambazo hazina michepuo yao.
Hii ni baada ya wanadunzi 1,189 waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini kubadilishwa na kupangiwa shule nyingine.
Kati yao, wanadunzi 865 wamepangiwa shule nyingine na 324 wamebadilishiwa shule kwasababu walipangwa kwenye shule ambazo hazina michepuo ya masomo yao waliotakiwa kwenda kusomea.
Haya yamebainika katika tangazo lililotolewa na katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kwenye tovuti ya wizara hiyo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tangazo hilo lilieleza kuwa baadhi ya wanafunzi hao wamebadilishwa michepuo (combination) na wengine shule, kwa sababu mbalimbali ikiwamo walioomba kubadili ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali.
"Wizara imepokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au combinations, walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara imetafakari maombi hayo na kufanya nabadiliko kwa wanafunzi wenye sababu zifuatazo....waliopangwa shule za kutwa nahali ambapo hawana pa kuishi; walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hispitali; walioomba kuhamia shule za kutwa kwa sababu za kiuchumi na walioomba kubadili combinations ambazo hazipo katika shule walizopangwa awali" Limesema tangazo hilo.
Tangazo hilo lilifafanua zaidi kwamba baada ya serikali kutangaza matokeo Julai 10, mwaka huu na kuwataka wanafunzi kuripoti kwenye shule walizopangiwa kabla ya Julai 29, mwaka huu, Wizara hiyo imepokea maombi ya wanafunzi kutaka kubadilisha shule au michepuo....
Soure...Gazeti la Nipashe.