strong ruler
JF-Expert Member
- Nov 2, 2013
- 4,921
- 3,305
Betri inapobaki asilimia ngapi ya chaji inafaa kuchajiwa tena?
Mwendo kasi wa kuchaji simu ya mkononi unabadilikabadilika. Baadhi ya wakati unaichaji simu yako kwa muda mfupi lakini inaweza kufanya kazi kwa muda mrefu, na baadhi ya wakati unaichaji kwa usiku mzima lakini betri inakwisha ndani siku moja. Basi katika hali gani betri inachajiwa kwa kasi zaidi?
Kwa kawaida betri isiyo na chaji inafanana na mtu mwenye kiu. Mtu mwenye kiu anakunywa maji haraka sana, na betri isiyo na chaji inachaji kwa ufanisi mkubwa zaidi. Wakati inapobaki asilimia 10 ya chaji, simu yako inapata mkondo mkubwa zaidi wa umeme kuliko wakati inapobaki asilimia 50 ya chaji.
Sasa unafikiri ni bora kuchaji simu yako wakati betri inapokaribia kwisha? Lakini kitendo hiki si sahihi. Katika miaka mingi iliyopita betri za simu za mkononi ni za aina ya NiMH.
Ni vizuri kuzichaji betri hizi baada ya chaji kwisha. Lakini siku hizi betri za simu za mkononi ni za aina ya Li-ion, kuzichaji wakati chaji inapokaribia kwisha kutaziharibu na kupunguza maisha ya betri. Betri inaweza kutumiwa kwa mizunguko kadhaa, baadaye inaharibika na haitaweza kutumiwa tena. Mzunguko mmoja unamaanisha kuchajiwa mpaka asilimia 100 na kutumiwa mpaka chaji inapokwisha.
Hivyo kama kila siku unaitumia simu yako mpaka chaji inakwisha, mizunguko ya betri inamalizika mapema. Hivyo ni bora kuchaji simu yako wakati betri inapokuwa chini ya asilimia 50.