Habari wakuu, mimi ni mvutaji wa sigara, sasa nataka kuacha kuvuta, ila nataka nibadli nitumie e-cigarette kwa mpito, naomba kujua hii e-cigarette kama inamadhara? Na kwa Tanzania ni wapi nitapata?
Kwa nini usiache jumla jumla mkuu..Mie nilitumia njia ya kunywa maji ya baridi sana kila ninapojisikia hamu ya kuvuta ni miaka mitatu sasa sijatia sigara mdomoni..
Huwa zinalipuka(Hii nimesoma kwenye Mitandao). Kiafya wanasema si Nzuri. Kama tatizo lako ni kuacha Sigara fanya kama mimi nilivofanya sababu hata mimi kuna wakati niliaanza kutumia hizo e-cigs lkn baadae nikagundua nazo pia ni kama Sigara tuu. Hivyo njia rahisi ya kuacha Sigara ni kuamua tu kuacha kwa kuanza kupunguza taratibu. Mimi sasa nina Mwaka sijagusa Sigara.