EL,AC na RA Fanyeni Haya

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Mh. Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz, sikilizeni ushauri wangu. Inawezekana mmeshapata ushauri mwingi na toka kwa watu mbali mbali. Mimi ninawashauri hivi, (kwa kuwa naamini mliyoyafanya/ au hamkufanya kwa ajili yenu tu, bali kwa ajili ya wenzenu):
  1. Jitokezeni hadharani, semeni ukweli wenu wote, msimung'unye maneno. Kweli milele humweka mtu huru.
  2. Mtubu mbele za Mungu wa Mbinguni na mbele ya watanzania kwa yote yaliyosemwa na yanayosemwa juu yenu
Mkifanya hayo, mtu yeyote atakayeinuka kuwasema atakuwa kioja. Msiiogope CCM,kwani ccm sio mlango wa kuingia mbinguni. Kumbuka, kama yanayosemwa juu yenu yote ni kweli, hamkuyafanya kwa ajili yenu, bali mliyafanya kwa ajili ya ccm au viongozi wa ccm. Sasa ni kwa nini ccm imewageuka kiasi hicho?

Fedha za EPA kwenda Kagoda inasemwa ndizo zilimwezesha JK na ccm kushinda uchaguzi wa mwaka 2005 na kwa sehemu fedha hizo hizo (mtaji huo huo) umewarejesha JK na ccm madarakani katika uchaguzi wa 2010. Ushindi huo wa mara mbili (2005/2010) wa CCM ulichangiwa na juhudi zenu binafsi. KIMANTIKI, KILA MWANA CCM ''wana-magamba' ALIYESHANGILIA NA ANAYESHANGILIA USHINDI HUO NA KULINGA NA KUTEMBEA KIFUA MBELE ANASHANGILIA FAULO MLIYOFANYA, NA ANATAMBA NA KUJISIFU KWA UOVU HUO.

SASA, INAKUWAJE ZIGO LOTE LA LAWAMA MTUPIWE NINYI WATATU TU? MIPANGO YOTE YA USHINDI NA NIKAKATI YA KUSHINDA ILIFANYIKA NA CC YA CCM ILIYAPA BARAKA. HILO ZIGO LA KUCHAFULIWA NI LAO WOTE
WANAOJIJUA NI WANA CCM.

Ninyi tubuni, hao wengine wabaki na zigo lao.
 
Kweli mkuu,kwa mfano RA aeleze jinsi alivyokwenda kufanya shoping ya zile karatasi za kura zilizokamatwa kule Tunduma,mbona ataoneka shujaa, fungukeni semeni yoooooooooooote.
 
Back
Top Bottom