Potatoes
Member
- Aug 26, 2016
- 78
- 79
Ufahamu wangu wa wastani wa lugha ya kiingereza na kiswahili umenifanya nione matumizi yasiyo sahihi ya either...or ya kiingereza na neno 'aidha' la kiswahili.
Nimegundua kwamba baadhi ya wazungumzaji wa kiswahili hufikiri kwamba either ...or ya kiingereza kiswahili chake ni aidha. Kwa hiyo nimewasikia hao wazungumzaji wa kiswahili wakisema: Wanaohusika na uchafu wa mazingira aidha ni wananchi au halmashauri za wilaya.
Ninawaonea huruma sana hao waswahili kwa kosa kubwa sana la kudanganyika na matamshi ya kiingereza ya either....or.. na kudhani ni aidha...au..!
Nimeisikia mara nyingi sana hii.
Wazungumzaji wengi wa kiswahili wamesahau kwamba kuna muundo wa 'ama.......au.....' ambao ndio tafsiri ya 'either.....or...'
Hiyo 'aidha' wanayoikimbilia ina maana tofauti kabisa katika kiswahili.
'aidha'=1.zaidi ya hayo.........
2.pia vilevile..........
3.kwa kuongezea.......
Wadau, mwasemaje.Nipo kwenye mstari au nimepotoka?