EFM, imekuaje Scorpion (aliyemtoboa mtu macho) kuwa huru?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Jina lake halisi ni Salim Njwete Salum, jina maarufu ni 'SCORPION' alijulikana zaidi kutokana na tukio la kumtoboa mtu macho. Alikamatwa na akahukumiwa kifungo. Sasa ametoka yupo mtaani na mengi yamezungumzwa kuhusu
yeye. Na bado wengine wanaendelea kumsema na kumuhukumu mtaani.

Najiuliza Kwa Tukio Alilo lifanya huyu Scorpion La Kumtoboa Mtu Macho na Kumpa Kilema cha Milele cha Kutokuona Yanayo endelea Duniani, Inakuaje ameachiwa huru?

Tuseme usalama wake utakuwaje huku mtaani? Mahakama na magereza Vitawaaminisha vipi wananchi kuwa huyu amestahili kutoka? Huku akimpa mtu Kilema Cha milele na muelekeo mbaya sana wa Maisha?

Lakini Pia EFM walitaka kumfanyia mahojiano leo, hii Radio Wamefikiria kweli?

Kumbe haya mambo yanawezekana unaweza fanya tukio Baya sanaa ukawa huru

IMG_2565.jpg

IMG_2563.jpg
 
Si walisema yule mwamba alietobolewa alkua anamiliki genge la vibaka kupora vitu mtaani mmoja wao akampora dadake scorpion jamaa akmuendea akamwambia arudishe mzigomwamba akawa mbishi.

Mwenye kukumbuka vzr hii story atukumbushe.
Mmhh ngumu mbona nasikia sio mmoja aliyemfanyia unyama? Then aliekatobikewa macho ripoti ya kitabibu ilionyesha hatoweza kuona tena na alikuwa Chini ya Paul Makonda kipindi hicho na Seriakali iligahalamia kuwekwa ata macho bandia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alietobolewa alishalalamika kabla huyo Scorpion kutoka. Mwenyewe alilalamika jamaa kutolewa kwa njia ya Parole kama sikosei. Alifuatwa na askari magereza kuombwa aridhie Scorpion atolewe sema alisikitishwa na issue hiyo kwani Usalama wake, na unyama aliotendewa anaona jamaa hastahilj mpaka amalize muda wake
 
Tatizo alietobolewa alikua anafadhili wezi kwa kununua vitu kutoka kwao, alionywa hakusikia.

Ni watu wangapi walidhurika na genge lake la Wizi?

kuna muda kama hutaki kuacha tabia flani, inabidi ulazimishwe kuacha
 
Ile story ilikuwa one sided! Jamaa alifanya ukatili ila palikuwa na sababu ya yeye kufanya huo ukatili..haikusemwa ama kuonekana wakati ule ila jamii inayowazunguka inatambua ukweli na siku zote anaeanza haonekani ila anayemaliza ndio huonekana mbaya.
 
Jina lake halisi ni Salim Njwete Salum, jina maarufu ni 'SCORPION' alijulikana zaidi kutokana na tukio la kumtoboa mtu macho. Alikamatwa na akahukumiwa kifungo. Sasa ametoka yupo mtaani na mengi yamezungumzwa kuhusu
yeye. Na bado wengine wanaendelea kumsema na kumuhukumu mtaani.

Najiuliza Kwa Tukio Alilo lifanya huyu Scorpion La Kumtoboa Mtu Macho na Kumpa Kilema cha Milele cha Kutokuona Yanayo endelea Duniani, Inakuaje ameachiwa huru?

Tuseme usalama wake utakuwaje huku mtaani? Mahakama na magereza Vitawaaminisha vipi wananchi kuwa huyu amestahili kutoka? Huku akimpa mtu Kilema Cha milele na muelekeo mbaya sana wa Maisha?

Lakini Pia EFM walitaka kumfanyia mahojiano leo, hii Radio Wamefikiria kweli?

Kumbe haya mambo yanawezekana unaweza fanya tukio Baya sanaa ukawa huru

View attachment 2059010
View attachment 2059012
stori ya huyu jmaa haikubalance,Makonda alifosi ionekane kama inavyoonekana lakini ukweli ni kwamba mtobolewa macho yule bwana ndio mhalifu mkubwa alistahili kwenda jela.....inasemekana eti Makonda alitaka jambo kwa scopion mwamba akachomoa ndo akaundiwa zengwe hadi akafungwa.
 
Ile story ilikuwa one sided! Jamaa alifanya ukatili ila palikuwa na sababu ya yeye kufanya huo ukatili..haikusemwa ama kuonekana wakati ule ila jamii inayowazunguka inatambua ukweli na siku zote anaeanza haonekani ila anayemaliza ndio huonekana mbaya.

ndiyo hapo sasa, angepewa nafasi asikilizwe ukweli ujulikane.

Nawachukia sana wezi, kukuua au kukupa Kilema kwao sio shida
 
stori ya huyu jmaa haikubalance,Makonda alifosi ionekane kama inavyoonekana lakini ukweli ni kwamba mtobolewa macho yule bwana ndio mhalifu mkubwa alistahili kwenda jela.....inasemekana eti Makonda alitaka jambo kwa scopion mwamba akachomoa ndo akaundiwa zengwe hadi akafungwa.
Naona mnataka kumsafisha huyo scorpion, the issue is whether alimjeruhi huyo mlalamikaji or not haya mambo mengine hayahusiki mahakamani.

Hata ukiua kibaka na ukakamatwa utapigwa kifungo Cha maisha au kunyongwa Hadi ufe haijalishi alikuwa mwizi.

All in all, huyo jamaa nae alikuwa mhalifu walikutana wote mabingwa wa uhalifu sioni sababu kwa nini apewe umaarufu kisa alikuwa mkabaji maarufu Hadi kutoboa macho watu. Imagine jamaa anatoboa mtu macho aisee huyu ni katili mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom